Changamoto za bei ghali ya bidhaa muhimu: Wakaaji wa Bungoma waelezea

0
16

Wakenya wanaendelea kukumbwa na hali ngumu ya maisha huku bei ya mafuta yakiathiri bei ya bidhaa na huduma muhimu ukaguzi wa haraka katika maduka yanaonyesha kuwa lita moja ya mafuta ya kupikia yanauzwa kwa shilingi mia tatu hamsini na saba ,kilo moja ya sukari kwa shilingi mia moja hamsini na tano,kilo moja ya unga wa mahindi shilingi tisaini na nane,kilo moja ya unga ngano shillingi mia moja na nne ilhali mililita mia tano za maziwa kwa shilingi hamsini na tano za kenya.

Je, kuna uhusiano upi baina ya bei ya mafuta na bidhaa muhimu? Vifurushi vya plastiki vya vyakula kwa mfano maziwa yanatengenezwa kwa mafuta ya petroli vilevile katika utengenezaji wa bidhaa katika viwanda upashaji wa moto unahitaji mafuta pia.

Gharama ya maisha inaendelea kupanda kila uchao si usafiri, bili za matumizi na hata bei mya vyakula na hali hii si sawia na ile ya miaka mitano iliyopita.licha ya haya,wakenya wamejizatiti kwa udi na uvumba kuweza kutafuta angalau kitu cha kutia kinywani.

Nilizuru mji wa Bungoma na kukutana na Haman Wafula muuza nafaka katika soko la kaunti ya Bungoma ambaye analalamikia kupanda kwa bei ya bidhaa. Anaongezea kuwa mambo yamebadilika kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na miaka ya hapo awali.

Kwa mtazamo wa mambo,ni dhahiri kuwa biashara nyingi hupita saa nyingi bila wateja hatua chache namkuta Kainnab Kassim muuzaji wa mitumba ambaye anasikitikia gharama kubwa ya maisha hasa kwa mafuta ambayo ni bidhaa muhimu.

Sasa hivi baadhi ya bidhaa sio kipaumbele kwa baadhi ya wakenya kutokana na kauli yake, hii ni taswira ya maisha magumu ambayo wakenya wengi wanakumbana nayo vilevile changamoto hizi zinadhihirika barabarani Thadeus Wambesho mhudumu wa bodaboda anasimulia changamoto anazokumbana nazo baada ya kupanda kwa bei ya mafuta.

Changamoto hizi zimewapelekea kuongeza nauli jambo lililopelekea wateja wao kukwepa huduma zao nilibadilisha njia na kuelekea kijiji cha Maliki eneo la Kibabii na kumkuta Mabele anayehudumu katika hoteli ya ugali na nyama ya nguruwe ambaye anasikitikia hali ngumu ya maisha, ugali ukiwa chakula kikuu nchini Kenya hasa Magharibi ya Kenya hivi sasa nyongeza ya ugali yani ugali sourcer haitolewi.

Na Emmaculate Wamalwa

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here