
Taasisi ya kimataifa ya kukabiliana na sera ya chakula IFRI imeonya kuwa mzozo wa mabadiliko ya tabianchi huenda ukazidisha ukosefu wa usawa kati ya wanaume na wanawake kote nchini.
Utafiti wa taasisi ya kimataifa ya sera na chakula duniani unaonyesha asilimia hamsini na moja ya shughuli za kilimo huchangiwa na wanawake, kujumlisha ufugaji wa mifugo hadi kilimo cha mimea. Wanaume kwa upande mwingine wanakumbatia mbinu mbadala za kujitafutia riziki kwa kasi zaidi kuliko wanawake.
Taasisi ya IFRI sasa inahofia uwezekano wa kuzidisha migawanyiko ya kijamii na kusababisha ukosefu wa usawa wa kijinsia Iwapo mfumo wa taarifa za kilimo cha kisasa haitahamasishwa miongoni mwa wanawake.
“Only 1/3 of women access mobile internet to actually use this information. Women also don’t have land titles and can’t sign up for the fertilizer subsidies. So, we need ways for women to learn from women on how to adapt to this multiple crisis.”
“Ni 1/3 tu ya wanawake wanaopata mtandao wa simu ili kutumia habari hii. Wanawake pia hawana hatimiliki za ardhi na hawawezi kujisajili kwa ruzuku ya mbolea. Kwa hivyo, tunahitaji njia za wanawake kujifunza kutoka kwa wanawake juu ya jinsi ya kukabiliana na mgogoro huu mwingi.”
Barack Okoba, mkuu wa mfumo wa chakula na maisha amedokeza kuwa pia utekelezaji wa kilimo bora kwa kutumia mfumo bora unaoweza kustahimili makali ya ukame na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na sio tu upungufu wa maarifa unamwandama mwanamke.
“When there is drought like it is, definitely the first culprit is the woman and children. And so maternal issues come in in hand that women will not have adequate food, not only to feed themselves but also to feed their children.”
“Kunapokuwa na ukame kama ulivyo, hakika muathirika wa kwanza ni mwanamke na watoto. Na hivyo masuala ya uzazi yanakuja mkononi kwamba wanawake hawatakuwa na chakula cha kutosha, sio tu kujilisha wenyewe bali pia kuwalisha watoto wao.”
Kulingana na Nancy Omollo mtaalamu wa masuala ya jinsia kuhusu mabadiliko ya hali ya anga, wanawake wanakabiliwa na changamoto katika kupata maarifa na teknolojia inayohitajika kujenga ujasiri wao dhidi ya masuala haya ya hali ya anga kama vile ukame na njaa.
Takwimu zilizotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa UN zinaonyesha kwamba asilimia themanini ya watu wanaohangaika kutokana na mabadiliko ya tabianchi ni wanawake na inachangiwa na vile jamii imemsawiri mwanamke kama mlezi wa jamii na kumfanya awe katika hatari Zaidi ukame unapotokea. Wadau wamehimiza sekta husika kuweka mikakati ambayo itajumuisha mwanamke. Ni wazi kwamba mikakati mingi humpendelea tu mwanamume na hivyo si sawa.
Na Calvin Angatia