
Shehena ya ngano kutoka nchi ya Ukraine imewasili katika bandari ya Mombasa. Balozi wa Ukraine nchini Andrii Pravednyk amesema kuwa tani hizo 54,000 zitasaidia taifa kukabiliana na uhaba wa chakula.
Hii ni meli ya kwanza kutia nanga bandarini baada ya vita vikali kuzuka nchini Ukraine mwezi Feburuari. Balozi wa ukraine andrii pravednyk amesisitiza kuwa wawekezaji wa Ukraine wako tayari kuwekeza katika nchi ili kuhakikisha kuwa kenya inasalisha chakula cha kutosha katika kukabili baa la njaa
“Sahii rais William Ruto pia alidakiza kuwa kuhakikisha kuwa kenya inajitosheleza kivyakula na kupunguza kupokea vyakula kutoka nchi za nje ni miongoni mwa ajenda zake.“ Andrii Pravednyk balozi wa Ukraine.
Balozi huyo pia amesema kuwa miongoni mwa agenda za Rais William Ruto ilikuwa ni kuhakikisha kuwa Kenya inazalisha vyakula vya kutosha ili kuthibiti upokeaji wa vyakula kutoka nchi jirani.
“Kenya inazalisha ngano lakini kutokana na sababu sisizoelezeka ngano hiyo huvunwa kwa viwango vya chini. viwango ambavyo haviwezi kuwatosheleza wakenya wote, hivyo basi nawaahidi kuwa kuna wataalau katika nchi ya Ukraine ambao wako tayari kushirikiana na kenya ili kuhakikisha Kenya inazalisha ngano si haba na sio ngano tu.“ Andrii Pravednyk balozi Ukraine.
Amesema kuwa licha ya ngano kuzalishwa nchini humu. ngano hiyo huvunwa kwa viwango vya chini sana na ambavyo havitoshi kuwafikia wakenya wote.vile vile ameahidi kuwepo kwa kampuni mbili zenye wataalamu nchini Ukraine ambao wako tayari katika kushirikiana na kenya ili kuzalisha ngano bora si haba.
Hata hivyo kutokana na namna hali ilivyo nchini kenya kwa sasa. kauli hii ya andrii inamwonekano wa kuleta afueni ya vyakula kwa wakenya wengi.
Na Juliet Wekesa