Hatimaye suluhu yapatikana kukabiliana na hali ya njaa nchini

0
12

Huku siku ya chakula ikiadhimishwa hapo juzi, wito ulitolewa kwa wananchi kuangazia vyakula vinavyostahimili ukame ili kukabiliana na janga la ukame lililokithiri humu chini na kuathiri mamilioni ya watu.

Siku hii huadhimishwa kwa malengo ya kuikumbusha jamii ya kimataifa jinsi baa la njaa halichagui yeyote bali inaathiri maskini na hata tajiri vilevile yaathiri nchi iliyosonga mbele kimaendeleo na ile iliyobakia nyuma.

Waanzilishi wa siku hii ni shirika la chakula na kilimo la umoja wa mataifa abao lilipania kukabiliana na baa la njaa lililoathiri mamilioni ya watu na uboreshaji wa mifumo ya kilimo .

Hivi sasa nchi nyingi duniani zinakabiliwa na baa la njaa ambalo limechangiwa na mabadiliko ya tabianchi ambayo huchangia pakubwa majanga kama vile ukame,mafuriko na ongezeko kubwa ya joto.

Gavana wa kaunti ya Siaya James Orengo amewahakikishia wakaazi hasa wakulima kuwa watafanikishiwa kupanda kabla ya disemba kwani hilo litasaidia ujenzi wa kaunti hiyo.

“Kaunti ya siaya kila mwaka inapata takriban billioni nane kila mwaka lakini kwa bahati mbaya billioni mbili pekee ndio inatumika katika maendeleo ilhali kaunti ya laikipia inapata takriban billioni tatu inayofanyia maendeleo “ alisema gavana James Orengo wataalamu wa udongo kutoka shirika la calro wamewarai wakaazi wa kaunti hiyo kutafuta usaidizi ilikuboresha udongo wao.

“Tunaeleza wakulima yakwamba wajaribu wasiwe watu ambao wakiumwa na kichwa wananunua dawa ya kuzuia maumivu hii inamaanisha ikiwa udongo wa kila mtu unasumbua tafadhali tujulishe sisi watu wa calro tupime na kukueleza jinsi unavyoweza kutekeleza kilimo,” alisema mtaalamu wa udongo.

Ukulima ukiwa uti wa mgongo wa nchi hii wakaazi hao wameraiwa kuipa ukulima kipaumbele katika kaunti hiyo.

Na Emmaculate  Wamalwa

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here