Afueni kwa waathiriwa wa wizi wa mifugo, Kerio, wabunge kuwasilisha mswada wa fidia.

0
1

Wabunge katika bonde la Kerio wamesema watapitisha mswada bungeni wa kuwalipa fidia walioathirika mara kwa mara na wizi wa mifugo hii ikiwa njia moja ya kuponya makovu ya majambazi.

Bonde hili la kerio linajumuisha kaunti tano ikiwemo kaunti ya baringo,elgeyo Marakwet, Westpokot , Turkana na Samburu na jamii inayopatikana sehemu hii ni jamii ya wafugaji.

Visa vya wizi wa mifungo na uvamizi umeripotiwa mara kwa mara katika bonde la Kerio huku ikichangia vifo ya mamia ya watu na umaskini baina ya wakaazi. Wabunge wa eneo hilo wadai kuwasilisha mswada bungeni ilikuwezesha waathiriwa wa wizi wa mifugo na uvamizi kufidiwa na serikali.

‘Tume kaa chini na kuanza kutengeneza sheria ya kufidia waathiriwa ambayo itaweza kusaidia watu wetu wapate fidia kutokana na mambo ya ukosefu wa usalama katika maeneo haya”alisema timothy toroitich.

Huku oparesheni ya usalama ikiendelea katika eneo hilo,viongozi hao wameisifia hali ya utulivu ambao unashuhudiwa sasa hivi huku wakiomba serikali kutoa msaada kwa wakaazi kwani vita viliathiri ukulima

“Tutasaidiana na wabunge,wakilishi wadi,maseneta na magavana kutoka mkoa huu kuhakikisha kwamba watoto wa tiati waweze kuenda shule bunduki itupwe na miaka kumi ijayo watoto wa huku waishi kama wakenya wengine na sisi watu wa Marakwet

Tumeumia sana” alisema wisley Rotich vilevile wameomba serikali kuimarisha miundo misingi katika eneo hilo kama njia moja ya Suluhu ya changamoto wanazokabiliana nazo hasa ya bwawa ya Kimwarer na Aror.

“Nataka kusihi serikali kuhakikisha bwawa ya aror, kimwarer na embugut imejengwa ndiposa maswala ya ukosefu wa usalama katika bonde la kerio iwezekukabiliwa kwa  kujihushisha na unyunyuzaji maji hata eneo la tiati ilikuwawezesha waende shule”alisema william kisang.

Na Emmaculate Wamalwa

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here