The Heiress kuchezwa kwa lugha ya kiswahili.

0
126

Mashabiki wa Tandao Tv Kenya wamerai mkurugenzi wa runinga hii Robert Wanyonyi kukipeperusha kipindi cha the Heiress katika lugha ya kiswahili, kipindi hiki kilianza jumatatu ya wiki hii katika ugha ya kimombo lakini kuanzia jumatatu ijayo kitakuwa kinapeperushwa katika lugha ya Kiswahili.

Kipindi cha “The Heiress” sasa kitakuwa kinapeperushwa katika lugha ya kiswahili kuanzia siku  ya jumatatu wiki ijayo. Hii ni baada ya mashabiki wa kubwa wa tandao kurai mkurugenzi wa Tandao Robert  Wanyonyi kuwa kipindi hicho kipeperushwe katika lugha ya kiswahili.

Katika mazungumzo na robert alisema kuwa madai ya mashabiki wake yatatekelezwa na mikakati iko njiani kwa ajili ya madai haya.aliguzia pia kuwa kuna vipindi vingine kama “The Brothers” pia vitakuwa  vikionyeshwa kuanzia jumatatu wiki ijayo runinga ya tandao ikijiunga na runinga zingine kupeperusha filamu za kimapenzi.

Mashabiki wa tandao wameiunda vikundi mbalimbali katika mtandao wa kijamii wa facebook ili  kuzungumzia kipindi hiki cha the Heiress na filamu zingine. Mkurugenzi wa tandao pia alisema runinga hii ya tandao itakuwa ikichukuwa mfumo mwingine ili kuimasrisha utangazaji wa habari kuanzia mwezi ujao.

Aliwasihi pia watazamaji hawa kujiunga kwa mawasiliano ya moja kwa moja kwa mkutano wa  google jumapili hii. Mkutano huo ambao utaanza saa sita hadi saa saba utakuwa wa kwanza kufanyika.

Mawasiliano hayo ya moja kwa moja yataguzia masuala mbali mbali, mkurugenzi wa tandao atakuwa akiyajibu maswali ya mashabiki wake na kuelezea kwa kina mfumo mpya ambao runinga hii utakuwa unachukua kuanzia mwezi ujao.

By Marion Wafula

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here