
Gavana wa Siaya James Orengo ametupilia mbali agizo la kusitisha malipo ya madeni kwa wanakandarasi waliojitwika majukumu ya kukamilisha miradi mbali mbali na kuagiza malipo hayo yafanywe haraka iwezekanavyo kulingana na sheria.
Wanakandarasi wa Siaya Orengo aruhusu wanakandarasi walipwe miradi ikaguliwe kabla ya malipo kufanyika gavana Orengo akihutubia katika bunge la Siaya amesema kuwa serikali yake imekaguwa stakabathi zote muhimu katika hazina ya kaunti hiyo na kufikia hatua hiyo ya kuwataka wanakandarasi walipwe ujira wao wa baada ya kujitolea katika kukamilisha miradi mbalimbali ya kaunti hiyo.
Aidha orengo amesema kuwa kuchelewesha kwa malipo hayo kunaathiri zaidi baadhi ya wanakandarasi na kuwafanya wengine wao kupata ugumu katika kutekeleza majukumu yao ya binafsi.
Hivyo basi orengo ametaka malipo ya wanakandarasi hao kukamilishwa kwa kufuatia ushahidi utakaotibitisha kukamilika kwa miradi iliyotolewa katika kaunti hiyo.
“We have an authorised payment of pending bills but there must be arecosd when you want to make a payment in a public institution, “ James Orengo says.
“There must be origination of a claim there must be a paper trale and when the payment is made there must be an acknowledgement in writing including stamps and seals that is the only way that the public or government money must or should be spend.“ James Orengo governor Siaya county.
Licha ya furugu kushuhudiwa katika kaunti mbalimbali kutokana na hali sawia na hii ya kusitishwa kwa malipo ya wanakandarasi miongoni mwa matukio mengine mengi.
Kaunti hii ya siaya inasemekana kudumisha amani miongoni mwao na zaidi wanaombwa kuendelea kudumisha amani hii ambayo ni adimu katika kaunti mbalimbali.
Wanakandarasi hawa ambao awali malipo yao yalisitishwa sasa wanaenda kupokea maluipo yao kutokana na kauli ya gavana James Orengo. Vile vile ni dhahiri kuwa malipo haya yatafanyika tu iwapo kutakuwa na shuhuda za kutosha zitakazoonyesha kuwa miradi hiyo ilifanyika na kukamilika kama ilivyoagizwa.
Na Juliet Wekesa