Wanyama pori waathirika kutokana na ongezeko la kiangazi nchini. Ukame! Je, sababu ni zipi?

0
3

Wanyamapori katika mbunga la kitaifa ya Tsavo wanakabiliwa na changamoto tele
ikiwemo uhaba wa malisho na maji inayochangiwa pakubwa na ukataji wa miti jambo
linalopelekea ukame unaohatarisha maisha yao.

Zaidi ya kaunti ishirni na mbili nchi zinakumbana na janga la ukame ambalo bado halijapata suluhu.
Katika mbunga la Tsavo, janga la ukame limepelekea uhaba wa malisho na maji ambalo limesababiasha
wafugaji kuvamia mbuga hilo kutafuta malisho huku wataalamu wakitahadharisha dhidi ya ongezeko
la joto Zaidi siku zijazo.

Mbunga hili ni kubwa zaidi nchini ilhali pia ni ya pili duniani baada ya mbunga ya Kruger iliyoko Afrika
kusini. Hifadhi hii imegawanywa katika sehemu mbili Tsavo mashariki na Tsavo magharibi na sifa zake
zimeboba kote duniani kwa uhifadhi wa wanyama maarufu watano chui,ndovu,kifaru, samba na nyati.
Mbunga la Tsavo limechangia pakubwa katika sekta ya utalii hapa nchini hivyo basi kupitia utalii uchumi
wa nchi yetu inanawiri. Uchumi husaidia katika ujenzi wa miundo misingi katika taifa kama vile
barabara,shule ,hospitali na kadhalika.

Ukame katika maeneo hayo yamesababisha wanadamu kujihusisha katika uwindaji haramu ilikupata
chakula baada ya mimea yao kunyauka kutokana na makali ya kiangazi.wanyama walio katika hatari
Zaidi ya kuwindwa ikiwa twiga ,swara na pundamilia.

“Tunaona ongezeko la joto na ukitazama data ya kihistoria ni wastani wa sentigredi ishirini na tano
lakini ifikapo mwaka wa elfu mbili na hamsini tutaona takriban nyuzi joto ishirini na saba nukta tano za
sentigredi na pia ifikapo mwaka wa elfu mbili na sabini tutaona takriban nyuzi joto ishirini na tisa nukta
tano”kulingana na wataalamu.

Uhaba wa chakula na maji imepelekea wanyama wengi kufariki kutokana na makali ya njaa na
kiu.wanyama wanatembea masafa marefu wakitafuta chakula na maji jambo linalowafanya kufariki njia, wanyama wanaoathirika zaidi na hali hii ni nyati na ndovu.

Mwaka huu kuna hofu ya moto kuzuka kufuatia ukame na shughuli za wafugaji kama ilivyo shuhudiwa
mwaka jana .chanzo ya moto hii ni mkwaruzo wa kwato za wanyama hao dhidi ya mawe inatoa miale ya
moto,pili wafugaji wanaovuta sigara kwenye mbunga hizi na kurusha mabaki hayo hushababisha moto.
Washikadau mbalimbali wameweka mikakati ya kuhifadhi maji msimu wa mvua itakayo tumika na
wanyama nyakati za kiangazi, wakulima wameweza kuhamasishwa umuhimu wa upandaji miti haswa
zile za kiasili aina ya mgunga (acacia).

“Hivyo tumeanzisha vitalu vyetu vya miti na pia tunashirikisha wateja wetu katika kupanda bolts za
mbegu . pia tumekubaliana na wakulima kwamba hatutatoa matangi ya maji ya plastiki kwa sababu
yanaweza kuharibiwa na tembo,” kulingana na washikadau.

By Emmaculate Wamalwa

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here