Busia yajipata katika dimbwi la ajira za watoto.

0
53

Mwito wa ushirikiano wa washika dau wote katika vita dhidi ya vitendo vya unyanyasaji na kufanyisha watoto kazi, ulitolewa katika kaunti ya Busia. Mashirika ya kiserikali na yasiyo ya kiserikali yameshirikiana kubuni mpango wa miaka mitatu unaolenga kufichua na kukabiliana na vitendo
vya kuwafanyisha watoto kazi katika maeneo bunge ya Teso Kaskazini na Matayos.

“We want to be fighters for children, we want to declare total war on the perpetrators of matters
to do with child labour in this county. Anyone messing up with a child is messing up with the
nation and we cannot allow that.” Sam Ojwang’
“Tunataka kupigania Watoto, tunataka kutangaza vita kamili dhidi ya wahusika wa masuala
yanayohusiana na ajira ya Watoto katika kaunti hii. Mtu yeyote anayecheza na mtoto anavuruga
taifa na hatuwezi ruhusu hilo.” Sam Ojwang’

Kamishna wa Busia Sam Ojwang alisema kwamba tayari wanajua wahusika na haitachukua
muda mrefu kabla ya kuwakamata. Alisema pia hawatakuwa na huruma na mtu yeyote
atakayejihusisha na suala hilo la unyama.
“From where I sit, working with the county government and those amongst us from the national
government who are involved in law enforcement and justice, it will be about taking action
against perpetrators.” Sam Ojwang.
“Kutoka mahali ninapoketi, nikishirikiana na serikali ya kaunti na wale miongoni mwetu kutoka
serikali ya kitaifa ambao wanahusika katika utekelezaji wa sheria na haki, itakuwa juu ya
kuchukua hatua dhidi ya wahusika.” Sam Ojwang.

Alisema kwamba atashirikiana na wanaohusiana na utekelezaji wa sheria na haki ili kuwatia
mbaroni wahusika. Hii ni kumaanisha kwamba atakayeshikwa atachukuliwa hatua ya kisheria na
kupelekwa mahakamani na hata kufungwa miaka mingi.

Kulingana na Magdalene Wanza ambaye ni mkurugenzi, shirika la terre de hommes, alisema
kwamba wako na rasilimali ya kutosha kushughulikia suala la ajira ya watoto.
“We have set up resources that we believe will be able to address the issue.” Magdalene.
“Tumetenga rasilimali ambayo tunaamini itasaidia kushughulikia suala la ajira ya watoto”
Magdalene.

Naye Beatrice Ogutu, afisa mtendaji wa ICS alisema kwamba wako na suluhu ya tatizo hilo.
Alisema ushirikiano wa mashirika ya kiserikali na yasiyo ya kiserikali utasaidia sana
kushughulikia suala la ajira ya watoto.

“We have solutions to this problem and action is no longer an excuse for all of us as we have
come together as partners I know we can pull our resources to take action. My urge for you and I
is that when you spot it, take action.” Beatrice Ogutu.

“Tuna ufumbuzi wa tatizo hili na hatua sio kisingizio tena kwetu sote kwani tumeungana kama
washirika najua tunaweza kuvuta rasilimali zetu kuchukua hatua. Ombi langu kwenu na mimi ni
kwamba mnapoiona, chukua hatua” Beatrice Ogutu.

Kutoka katika kaunti hiyo, tunashauriwa kutojihusisha na masuala ya kuwaajiri watoto kwani
utachukuliwa hatua ya kisheria

By Calvin Angatia

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here