
Tume ya mipaka na uchaguzi IEBC imetangaza rasmi tarehe ya uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika katika maeneo nane ya uakilishi hii ikitarajiwa kufanyika tarehe nane mwezi wa Disemba 2022.
Maeneo nane ikiwemo kaunti ya bungoma ambayo inafaa kushiriki uchaguzi huo baada ya aliyekuwa seneta wa kaunti hiyo moses masika wetangula kupata wadhifa wa spika katika bunge la kitaifa. wanaomezea mate kiti hicho wakiwa aliyekuwa mbunge wa bumula Mwambu Mabonga, Jacob Machacha Majembe, Martin Ndiwa,Bonewayne Nyongesa ,bishop Kasili,Joseph Lendrix Waswa, Aggrey Namisi, Moses Nandalwe, Ken Wafula, Kasembeli Nasiuma na David Wafula Wakoli.
Maeneo bunge yanayotarajiwa kushiriki uchaguzi huo ikiwa Nairobi city, Kakamega na kauntii ya Siaya vilevile mawodi kadhaa ambayo waaniajiwa wao walifariki ikiwemo wodi ya utawala,mumias kaskazini kaunti yua kakamega gem kusini kaunti ya siaya oloimasani kaunti ya narok ,kyome katka kaunti ya kitui yatarajiwa kushiriki katika uchunguzi huo mdogo.

Siku ya vyama kufanya mchujo na kuchagua watakao gombea kupitia katika tiketi chao ni tarehe kumi na tisa mwezi wa oktoba mwaka huu tume hiyo inatarajiwa kuchapisha rasmi majina ya wataogombea nyadhifa mbalimbali katika uchaguzi huo katika gazeti la serikali siku saba kabla ya kila kitu kuwekwa wazi kampeni za wataochapishwa kwenye gazeti hilo lafaa kuanza tarehe tisa November hadi tarehe sita Disemba mwaka huu kwanzia saa moja asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni , huku tarehe saba na nane imetengwa kwa mapumziko .
Wanaomezea mate nyadhifa mbalimbali wameamrishwa kutuma nembo ya vyama vyao kabla ya tarehe kumi na tatu huu mwezi.
Na Emmaculate Wamalwa