CBC kusitishwa!!!

0
37

Mwenyekiti wa kamati ya elimu na ambaye ni gavana wa kericho Dkt Eric Mutai  anaitaka wizara ya elimu kusitisha mpito wa wanafunzi wa daraja la sita kuingia shule ya upili ya ngazi ya chini. Amedai kwamba wallimu wa shule ya upili hawajajiandaa ifaavyo kuwafundisha wanafunzi walioko chini ya mtaala wa CBC.

Aidha Mutai amesema kuwa  miundo msingi kwenye shule za sekondari ni duni. Haziwezi kuwapokea wanafunzi wote wa wa daraja la sita na vile vile amesema kuwa walimu wa sekondari hawajajiandaa ipasavyo ili kuwafundisha wanafunzi hawa walio chini ya mfumo wa CBC. Pia ameisihi serikali kuwapa walimu muda mwafaka ili wajiandae tayari kuwapokea wanafunzi hawa wa CBC. 

`` Swali tunalouliza ni jinsi gani wizara imejiandaa sawa. Kwa sababu kwa ufahamu wangu sekondari ndogo inatakiwa kuwa ya nyumbani katika shule ya upili. Shule za upili tulizonazo hazina uwezo sawa. Walimu hawako tayari kushughulikia viwango hivyo vya wanafunzi. tunaomba wizara isimame kidogo na CBC. Simamisha CBC kwa muda na upe nafasi ya kushauriana na kufanya uamuzi wetu``

Mwenyekiti wa kamati ya elimu Dkt Eric Mutai tangu mwanzo wa serikali ya rais Ruto. Wakeya wamekuwa kwenye njia panda kutaka kujuwa iwapo mafunzo ya mfumo wa  CBC  yangesitishwa au la. Swala hili liliishia kutawanya baadhi ya wakenya kwani kuna wale walioshikilia mfumo huo kupigwa marufuku huku wengine wakidai mfumo huo usalie. Rais William Ruto baadaye alizindua jopokazi la CBC  ambalo linafuatilia mfumo huo kwa kushirikiana na rais na kubaini kama mfumo huo ungesitishwa au la. aidha jopokazi hilo linaendelea kufanya utafiti.  

By Juliet Wekesa

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here