“Ameamua kuwa mahakama, spika na msajili,” Wetangula akashifiwa.

0
54

Spika wa bunge la kitaifa Moses Wetangula ametoa uamuzi kwamba mrengo wa Kenya Kwanza ndio muungano wa walio wengi bungeni ikiwa na wabunge mia moja sabini na tisa huku mrengo wa Azimio la Umoja ikiwa na wabunge mia moja hamsini na saba jambo ambalo halikupokelewa vyema na wabunge wa mrengo wa azimio.

Katika uamuzi huo uliochukua Zaidi ya saa moja spika wa bunge la kitaifa alitoa hoja yake iliyopelekea uamuzi wake wa idadi ya wabunge wa azimio yapungue kutoka mia moja sabini na moja hadi mia moja hamsini na saba huku akielezea kuwa wanachama kumi nne waliondoka kutoka mrengo wa Azimio na kujiunga na Kenya Kwanza jambo ambalo lilifanya idadi a mrengo wa Kenya Kwanza kuongezeka kutoka mia moja sitini na tano hadi mia moja sabini na tisa.

Wetangula aliongezea kwamba hakuna mbunge aliyechaguliwa wala kuteuliwa kuwa mbunge kwa tiketi ya Azimio bali ni wale wa vyama mbalimbali vinavyounda chama cha muungano huo.

“Kwa maoni yangu haitakuwa busara katika nafasi za wajumbe kumi na wanne waliochaguliwa chini ya UDM,PAA, Maendeleo Chapchap na Movement for Democracy and Growth kama muungano wa chama ambao umejitenga na vyama vyao na hivyo basi kushawishika kuwa wanachama na vyama vyao ni wa muungano wa Kenya kwanza “ alisema spika Wetangula.

Tamko hilo halikupokelewa vyema na wabunge wa mrengo wa Azimio la umoja huku mbunge wa Ugunja Opiyo Wandayi ambaye pia ni kiongozi wa wachache katika bunge hilo la kitaifa kupinga uamuzi wa spika Wetangula alipuuzilia mbali madai ya mbunge huyo huku akielezea kwamba uamuzi wake ni wa mwisho na haliwezi likajadiliwa. Jambo hili lilianzisha mzozo baina ya wabunge wa Azimio la umoja na Kenya kwanza jambo ambalo lilipelekea spika kukamilisha kikao cha bunge hilo na kuelekeza kuwa kikao kitafanyika wiki ijayo tarehe kumi na tatu.

Baada ya hayo wabunge wa mrengo wa Azimio wakiongozwa na mbunge ugunja Opiyo Wandayi,mbunge wa Suna mashariki Junet Mohammed na John Mbadi wa Suba Kusini walizungumza na wanahabari huku wakielezea kutoridhishwa na uamuzi huo. “Haya mambo yamo katika katiba ya mahakama na ameamua yeye ndiye mahakama, msajili na ndiye Spika na sasa hii ni siku ya giza sana kwa nchi yetu,” alisema Junet Muhammed. Katika upande huo mwingine wabunge wa Kenya kwanza wakiongozwa na kiongozi wa wengine Kimani Ichungwa wamesherekea uamuzi uliotolewa na spika wakidai alitumia hekima ki.suleimani.

Story by Marion Wafula

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here