“Tulitia sahihi kwenye karatasi tupu,” Chama cha UDM cha jiondoa Azimio.

0
15

Katika kikao cha kwanza cha bunge la kumi na tatu likiongozwa na spika wa bunge la kitaifa, Moses Wetangula, mbunge wa Mandera North alijitokeza, na kusema kuwa walitia sahihi kwenye karatasi tupu ili kujiunga na mrengo wa Azimio la Umoja One Kenya

Huku vikao vya bunge vikiendelea, wabunge mbalimbali wameonekana kujitokeza na kupeana hotuba zao kulingana na vikao hivi, mbunge wa mandera kaskazini abdullahi bashir alihutubia bunge la kitaifa linaloongozwa na Moses Wetangula.

Bashir alianza hotuba yake kwa kuwakukumbusha wanchama wa udm kuwa mtu yeyote ana haki ya kuwa katika chama chochote kama ilivyonukuliwa katika katiba ya kenya. Alihutubia bunge kuu kuwa karatasi ziliwakilishwa kwa katibu tarehe kumi na mbili mwezi wa tatu katika jumba la makongamano kicc hazikuwa sahihi.

“Karatasi zilizowasilishwa kwa katibu tarehe kumi na mbili zinasemekana zilikuwa tupu, ni ukweli kwa sababu tulitia sahihi kwenye karatasi ambazo hazikuwa na maandishi yoyote kwa kutishwa na kulazimishwa”

Bashir ambaye ni naibu wa kinara wa chama cha udm alijitokeza na kudai kuwa walitia sahihi kwenye karatasi isiyokuwa na maandishi yoyote kwa kulazimishwa na kutishwa ili kujiunga na mrengo wa azimio la umoja one kenya unoongozwa na raila odinga.

Wanachama wa UDM walijiuzulu kwenye mrengo wa azimio baada mojawapo wa sababu wa kujiuzulu ni baada ya mmoja wao kuitwa majina na baadhi ya wanachama wa azimio la umoja wakati wa kampeni kuu alipokuwa kaunti ya siaya.

Bashir alidai kuwa chama cha UDM kinauwezo na kina nguvu kwa sababu wanachama nane wako katika bunge la kitaifa na watatu katika seneti na uongozi wao ni dhabiti na sasa wamejiunga rasmi na mrengo wa kenya kwanza unaongozwa na rais wa jamuhuri ya Kenya William Ruto

“Na rasmi tumejiunga na mrengo wa kenya kwanza, karatasi hizo zimewasilishwa kwa katibu na mimi kama naibu wa kinara wa chama cha udm niilishuhudia karatasi hizo zikitiwa sahihi”

Mbunge huyo alishtumu mrengo wa Azimio kwa uongozi mbaya na kutenda vibaya baadhi ya viongozi wa mrengo wa Azimio.

Na Marion Wafula

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here