
Walimu kote duniani wanaadhimisha siku yao, walimu nchini wamejumuika katika chuo cha mafunzo cha serikali eneo la lower kabete kaunti ya kiambu kauli mbiu ikiwa ni mageuzi ya elimu kuanza na walimu wenyewe. Sekta ya elimu ikiwa mojawapo ya sekta muhimu nchini ambay o hutoa ufahamu kuhusu kitu fulani hivyo basi hukuza vipaji na kupachika maarifa kuhusu taaluma nyingi kama vile udaktari,ualimu na kadhalika.
Kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa mageuzi ya elimu kuanza na walimu wenyewe baadhi ya walimu akiwemo mwalimu mkuu wa shule ya upili ya Lodwar Patrick Lokwagen ameelezea changamoto yao kutokana na hali ya ukame na changamoto za usalama lakini licha ya hayo jukumu lao limesaidia pakubwa katika kutunza jamii
“ Huwezi kuza tabia ya mtoto ikiwa tabia yako mwenyewe iko na kasoro ivyo basi walimu
Wafaa kuwa kipaumbele kwa kila jana iliwaweze kuigwa na watoto.ni vigumu sana
Kumrekebisha mtoto ilhali mienendo yako mwenyewe ni mbaya.” Patrick alisema walimu haswa katika sehemu ya kaskazini mashariki mwa kenya wamepitia na wanaendelea kupitia changamoto tele huku ikibainika kwamba sehemu hiyo imekumbwa na ukame kwa muda mrefu pia inashuhudia changamoto za usalama.
Tangu awali walimu wamelalamikia hali ngumu ya kikazi wengine wakilalamikia mshahara mdogo,mazingira mbovu za kazi huku wakilaumu serikali kwa kupuuza maslahi yao licha ya wao kukuza msingi wa mwanafunzi yeyote. Katika hafla hiyo katika kaunti ya kiambu, kahi indimuli mwenyekiti wa chama cha Wakuu wa shule za upili ameelezea kuwa walimu ni watu wa kuaminika sana nchini Kwani matokeo yao hudhihirika wazi baada ya muda mchache.
Kwenye hafla hilo pia hospitali ya medihill wameunga mkono kauli mbiu na kuahidi Kuungana nayo ili kuhakikisha afya nchini inapatikana kwa urahisi na kwa bei nafuu. Haya yataboresha masomo nchini kwani walimu na wanafunzi watamudu kukijikimu kiafya.
“Walimu ni watu waaminifu sana nchini kwani alama wanazopatia wanafunzi katika shule za upili huashiria wanavyoendelea katika vyuo vikuu.wahadhiri katika vyuo vikuu hutayarisha mitihani na kisha kusahihisha jambo ambalo wanatekeleza kwa uaminifu.”Kahi indimuli alielezea.
Tume ya elimu tsc hivi leo wamewatuza baadhi ya walimu kwa kazi nzuri waliofanya ya kuwatayarisha vyema wanafunzi wa mwaka jana waliofanya vyema kwenye mtihani wa kitaifa. Hii ni njia mojawapo ya kuwapa walimu motisha ilikutekeleza majukumu yao ipasavyo.
Na Emmaculate Wamalwa