Mwanafunzi ajitia kitanzi Kericho baada ya kuadhibiwa vikali na mwalimu.

0
11


Mtahiniwa wa darasa la nane katika shule ya msingi ya St. Theresa, Kericho alijitia kitanzi kwa kujining’iniza katika bafu moja ya shule hiyo. Matukio haya yalitokea tarehe ishirini na saba mwezi wa Septemba.

Kulingana na babake, inasemekana kwamba Enock Kipkoech aliadhibiwa vikali na mwalimu mmoja kabla ya kulazimishwa kwenda kuoga. Babake amejiuliza maswali asipate majibu.

“Kwa hiyo ni nani aliyemuua mtoto wetu, hilo ni swali tunajiuliza, yule aliyempiga kijana wetu, aliyemnyonga kijana wetu na kwa nini aliambiwa aende bwenini kuoga, haiwezi kumaanisha kitu kwetu,” babake alisema.

Wazazi wake walielekea katika kituo cha polisi cha Kericho kutafuta majibu ya kiini cha mwanao kujitia kitanzi. Richard Syele mbaye ni babake Enock alieleza kwamba licha ya ripoti ya upasuaji wa mwanawe kuonyesha kwamba alijitia kitanzi, mwili wake pia ulikua na alama, kuonyesha kwamba alichapwa.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo alieleza kwamba suala hilo liliweza kushughulikiwa na liliripotiwa. Alieleza kwamba aliitwa katika kituo cha polisi na akaandikisha ripoti kuhusu matukio hayo.

“OCS alinishauri niende kurekodi taarifa, ambayo nilifanya, na baada ya kurekodi taarifa hiyo nilirudi nikiambatana na maafisa wa polisi…” Alisema.

Ni wazi kwamba kesi zinazohusiana na mambo kama hayo huwa hazishughulikiwi vyema na serikali. Hii ni kwa sababu majibu huwa hayapatikani. Maafisa wa polisi husema tu watafanya uchunguzi ila hawaleti majibu.

Iwapo ni kweli mwanafunzi huyo aliadhibiwa vikali kulingana na madai, swali ni je, walimu wanaruhusiwa kuwaadhibu wanafunzi kwa njia hiyo au walipigwa marufuku? Walimu siku hizi hawaruhusiwi kuwaadhibu wanafunzi kwa kiwango fulani na mwalimu aliyehusika kwa matendo hayo anapaswa kuchukuliwa hatua.

Kulingana na mamake, Enock aliwai kuja nyumbani akilalamika kwamba walimu wanawachapa sana kuleshuleni. Aliomba wazazi wake wambadilishe shule kwa sababu ya vichapo hivyo.

“Kuna wakati alikuwa analalamika kuwa wanachapwa na mwalimu, Hata kuna wakati alikuwa
anasema atafutiwe shule nyingine…”

Uchunguzi wa kina umeanzishwa ili kubaini kiini kamili cha matukio hayo. Maafisa wa DCI wameanzisha upelelezi wao kwa undani kabisa ili kuhakikisha majibu yamepatikana na wazazi wa mwanafunzi huyo kuridhika.
Familia ya Enock Kipkoech imeanza kuandaa mazishi ya mwanao ili kumpumzisha. Wameapa kwamba watahakikisha aliyehusika amechukuliwa hatua za kisheria.

Na Calvin Angatia

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here