Je, unafahamu Sodoma na Gomorah ya Kanduyi?

0
121

Ni mji ambao kwa umbali, na kwa mgeni yeyote unaonekana tulivu, usio na mambo mengi, labda biashara ya bidhaa, mboga  na matunda nyakati za mchana. Taswira hii hata hivyo, inabakia mchana tu, nyakati za usiku zikifika, mambo yanabadilika.

Kanduyi mji unaopatikana kando kiasi na mji wa Bungoma, ikiwa kwenye barabara kuu ya kutoka Eldoret-            Webuye-kuelekea Malaba, mpakani mwa mataifa ya Kenya na Uganda na vile vile kwenye mataifa ya maziwa makuu.

Ni mji ambao  unapendwa sana kutembelewa na madereva wa malori yanayosafiri kutoka bandari ya Mombasa kuelekea Uganda na mataifa mengine. Mienendo hii ya madereva wa malori imefanya mji mkubwa wa Bungoma kukosa shughuli,  haswa nyakati za usiku. Ukilinganisha miji mingine katika eneo la magharibi, Kanduyi inapiku yote kutokana na bishara za usiku.

Punde tu ifikapo saa moja za usiku, Kanduyi huwaka an akina dada ambao, shughuli zao mingi hufanyika usiku.

Kuna mtindo mpya hapo, ambao hata malori jinsi yanavyoegezwa utashangaa, vile vile yanatumika kama nyumba vya kukodi kwa muda. Hapo utakumbana na mwanaume amekabiliwa na wanadada wawili ama zaidi. Wanadada hao hutumia uwepo wa giza totoro kando ya malori hayo kama chumba cha kuwa shughulikia wateja wao.

Wanaume wanapofika eneo hilo, hutumia muda mwingi kupiga bei, na hapo akina dada wasio na uvumilivu huwaambia waendelee kutafuta, maanake hao swala bei  iliyowekwa ni muhimu.

Jinsi madereva wa malori hayo huyaegesha, ni kama kwa mpangilio maanake yanapangwa yakiangaliana bila hatakuacha nafasi ya mguu kupita, na hivyo inaelekea ni sharti ambalo wameambiwa na akina dada hao wa usiku.

Makala yameandaliwa na Robert Wanyonyi

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here