
Viongozi kutoka kilifi ambao wanaegemea chama cha PAA wamemsuta kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka kufuatia kauli yake ya hapo awali iliyokashifu baraza la mawaziri lililoteuliwa na rais William Ruto akiwemo Aisha Jumwa. wamesema kuwa Kalonzo akae mbali na Aisha Jumwa kwani ndiye mwanamke wa kipekee baina ya Mijikenda kupata wadhifa huo tangu kuzinduliwa kwa ugatuzi.
Siku chache zilizopita kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka alilihujumu baraza la mawaziri lililoteuliwa na rais william Ruto akisema baadhi ya walioteuliwa wana madoa kufuatia kesi mahakamani akiwemo Aisha Jumwa.
Wakizungumza katika hoteli moja mjini kilifi. viongozi wa PAA wamemkanya Kalonzo dhidi ya matamshi yake ya hapo awali yaliyonuwia kukashifu hatua ya rais kuwateuwa baadhi ya mawaziri wakisema kuwa matamshi hayo yanawabaguwa wapwani wamesema kuwa Aisha Jumwa anahaki kisheria kukabidhiwa wadhifa huo kwani bado mahakama haijakiri kuwa anahatia.
“Kwa wakati wa kwanza kabisa kilifi imepata waziri mwanamke na tunamshukuru kwa sababu katika ile serikali iliyopita watu wa kilifi tulionewa hakuna waziri hata mmoja aliyechaguliwa kama ndani ya kilifi hatukupata waziri hata mmoja,“ alisema mmoja wa viongozi wa PAA.
Viongozi hao wamewataka wanaohusika na matamshi yanayoendeleza ubaguzi dhidi ya mawaziri wateule wa rais wasubiri hadi bunge lifanye maamuzi ya mwisho. Na kufika sasa mawaziri wapya hawajaanza kufanya kazi huku wakisubiri kuidhinishwa na bunge la kitaifa
kauli ya kiongozi wa wiper Kalonzo Musyoka ya hapo awali ya kumshtumu Aisha Jumwa na Mithika Linturi kuwa wanakabiliwa na kesi mahakamani na kuwa hawakustahili kuteuliwa kama mawaziri hivi majuzi zimekanushwa na naibu wa rais Rigathi gachagua kuwa kesi hizo ni za kuekelewa.
“Kama wewe unaishi kenya unajuwa hii kesi yote imekuwa yakuwekelewa. hata mimi mwenyewe niliwekelewa kesi. kesi iko na mithika linturi ni ya kuwekelewa aliwekelewa na george kinoti. kesi iko na aisha jumwa ni yakuwekelewa. sisi hatuwezikubali kukataza mtu ambaye ako na nafasi ya kuchangia maendeleo ya kenya kwa sababu ako na kesi ya kuwekelewa”
Rigathi Gachagua naibu rais aidha Gachagua alichukuwa fursa hiyo na kuishtumu serikali ya hapo awali ya rais uhuru kenyatta akisema kuwa. serikali hiyo ilishindwa kupanga siasa kwani ilikuwa na mawasiliano duni na wanasiasa na kuamua kutumia vitengo vya DCI na EACC kupanga serikali jambo ambalo liliwaweka mbali wanasiasa na kulazimika kufuata uamuzi wa serikali.
Hata hivyo wakaazi wa kilifi wameamua kukanusha madai ya kinara wa wiper na kusema kuwa wanajivunia uteuzi wa aisha jumwa kama waziri kwani ndiye mwanamke na waziri wakipekee kuteuliwa kutoka kilifi tangu uzinduzi wa ugatuzi. Pia wamemuahidi rais william ruto kuwa wako tayari kufanya kazi nae na iwapo kuna wale wanaokashfu uteuzi wa rais wa mawaziri. wasubiri hadi pale ambapo bunge litafanya maamuzi ya mwisho.
by Juliet Wekesa