
Muhoozi Kainerugaba, mtoto wa rais wa jamhuri ya Uganda ameondolewa katika nafasi ya kamanda wa vikosi vya nchi kavu vya jeshi la ulinzi la wananchi wa Uganda baada ya kutishia kushambulia nchi ya Kenya kwa maongezi yake katika mtandao wa kijamii wa twita.
Kamanda huyo wa zamani wa UPDF Muhoro, mwanawe rais wa nchi ya Uganda Yoweri Museveni aliandika kwenye mtandao wa kijamii wa twita utata kuhusu demokrasia nchini Kenya, kutoka kwa maoni kwamba rais wa zamani Uhuru Kenyatta alipaswa kugombea muhula wa tatu. Pia aliandika kuwa watavamia nairobi yeye pamoja na jeshi lake’
“Nitalivamia jiji la Nairobi na jeshi langu majumaa mawili yajayo”
Wizara ya mambo ya nje ya Uganda, hata hivyo, ilijitenga na maandishi haya kwenye mtandao wa twita ambao ulisababisha ghasia nchini kenya na vita katika mtandaonwa twita baina ya nchi hizi
Wizara hiyo ilisema kuwa hio serikali ya jamhuri ya Uganda inapenda kusisitiza ahadi yake ya ujirani mwema, kuishi pamoja kwa amani na ushirikiano
“Serikali ya jamuhuri ya Uganda inapenda kusisitiza ahadi yake ya ujirani mwema amani na ushirikiano”
Wizara ya mambo ya nje inapenda kufafanua kuwa serikali ya jamhuri ya uganda haifanyi sera yake ya mambo ya nje na shughuli nyingine rasmi kupitia mitandao ya kijamii wala haitegemei vyanzo vya mitandao ya kijamii katika kushughulikia serikali nyingine huru,” ilisema wizara hiyo.
Na Marion Wafula