Rais William Ruto aongoza ufunguzi wa bunge.

0
1

Ufunguzi wa bunge la kumi na tatu

Baada ya uapisho wa wabunge wa seneti na bunge na uchaguzi wa maspika wa bunge na seneti kote nchini ufunguzi wa kikao cha bunge ya 13 umefunguliwa rasmi na rais wa jamuhuri ya Kenya William Ruto hafla hiyo ilifanyika katika bunge kuu jijini Nairobi.

Wabunge wote nchini kenya ikiwemo wale wa mrengo wa upinzani walikusanyika katika bunge kuu jijini Nairobi kwa ufunguzi wa bunge la kumi na tatu.

Hafla hiyo iliongozwa na rais William Ruto ikiwa ni mkutano wake wa kwanza na bunge la kumi na tatu baada ya uapisho wake kuwa rais wa kenya katika uwanja wa michezo wa Kasarani.

Katika hutoba ya rais William Ruto aliwapongeza wabunge na mspika wa majumba yote mawili waliochagliwa na kuteuliwa kuongoza wananchi ya Kenya “kwa hiyo, nachukua nafasi hii maalum kuwapongeza nyote kwa kuchaguliwa kwenu katika uchaguzi mkuu uliopita na uteuzi uliofuata.imani iliyoonyeshwa na wakenya kwetu na taasisi zetu inapaswa kututia moyo kuinua kiwango cha utumishi wetu kwa taifa na uwajibikaji kwa wapiga kura. “

Aliwaambia kuwa wana wajibu wa kukomboa ahadi ya uchumi wa mwanchi wa kawaida. Baadhi ya  ajenda  alizoahidi kutekeleza  kwa msaada wa bunge hili la kumi na tatu ni maji, umeme na chanzo cha afya kiulimwengu

 “Serikali inaweza kutoa hili hatua kwa hatua, lakini sekta binafsi inaweza kuhamasisha yote mara moja. Kwa hivyo tutapitisha mfumo wa PPP kwa kuingia mikataba ya ununuzi wa maji na wawekezaji. Kwa njia hii, tutafikia maji kwa wote chini ya muongo mmoja. Kuhusu umeme, tutawezesha uundaji wa mbinu bunifu na madhubuti ili kutoa mifumo bora ya nje ya gridi ya taifa, ikiwa ni pamoja na kuwawezesha watumiaji kuunda vyama vidogo vya ushirika kwa ajili hiyo”.

Wananchi wa kenya wana matarajio mbalimali baada ya ufunguzi wa bunge ya kumi na tatu, baadhi ya wakaazi wa Webuye kaunti ya Bungoma waliwarai wabunge kutimiza ahadi zao walizowahidi wakati wa kampeni, waliomba wabunge hawa kuwawasilisha vyema katika bunge na kuwasilisha masuala yao kama hali mbaya ya uchumi iliyosababisha gharama ya maisha kuenda juu.

Na Marion Wafula.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here