Malkia waiponda Cameroon, afueni Stamford Bridge-Kante arejea mazoezini.

0
5

Malkia waiponda Cameroon

Malkia strikers walipata ushindi wao wa kwanza katika michuano ya kusaka ubingwa wa dunia katika mchezo wa voliboli nchini Uholanzi baada ya kucharaza wapinzani wao wa muda mrefu Cameroon seti 3 kwa sufuri. Vipusa hao walishinda kwa 25-20 kwa raundi ya kwanza, ya pili 27-25 na ya tatu 25-19. Malkia strikers na timu ya Cameroon wamekuwa wakiongoza michuano ya voliboli Afrika na kuliwakilisha vyema bara hili katika mashindano ya Olimpiki ya mwaka wa 2018 miongoni mwa mwashindano mengine. Licha ya kukaribishwa kwa kichapo na timu ya taifa ya uholazi, wanadada hao wangali na matumaini ya kufuzu katika kundi lao ikiwa wataadhibu mabingwa wa bara uropa italia na taifa la Puerto Rico.

Kante arejea mazoezini.

NKOLO

Chelsea imetangaza rasmi kupitia kwa tovuti yake kuwa Ngolo Kante amerejea mazoezini. Kiungo huyo amekosa mechi sita mfululizo za mwisho za Chelsea kufuatia kuuguza jeraha alilopata kwenye mechi kati ya Chelsea na Tottenham Hotspurs na hivyo kuondoka ugani kipindi cha pili. Wachezaji wengine waliorejea mazoezini ni pamoja na walinda lango Edouard Mendy na Kepa Arrizabalaga, mshambulizi Aubameyang, beki Chalobah na Loftus Cheek.hadi kufikia sasa Chelsea wamo katika nafasi ya saba baada ya kucheza mechi sita huku wakishinda mara tatu, kupoteza mara mbili na kupiga sare moja.

Na Brian Simiyu

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here