
Fununu za kuwepo kwa unyakuzi wa ardhi zimeibuka mjini Mombasa pale ambapo baadhi ya wanaharakati wamekashifu kuekezwa kwa uwa katika mzunguko ulioko Railways mjini Mombasa
nyakuzi wa ardhi.
Akiongoza waandamanaji hao mwanaharakati Bradily Ouna alisema kuwa wanahofia sana endapo ardhi hiyo tegemezi itanyakuliwa na bwanyenye huyo kwa kizingizio cha huduma kwa jamii iliyoko katika maeneo hayo
Vile vile mwanaharakati huyo Bradly pamoja na mfanya biashara mmoja wamekiri kuwa baadhi ya wafanya biashara walifungiwa biashara zao huku muhusika wa tuhuma hizi akitumia ardhi ya UMMA katika kuwakandamiza watu wengine
Hata hivyo kampuni inayosutwa imekana madai hayo huku mwakilishi wadi wa Chuudabonabalo akisema mwekezaji huyo wa kibinafsi alikabidhiwa sehemu hiyo na kampuni nyingine tajika ili atowe huduma kwa jamii kama vile kuwalisha wenye uhaba wa chakula.
Kulingana na baadhi kipande hicho cha ardhi kimekuwa kikitumika kama eneo la kuwalisha wasiojiweza na kusema hakijanyakuliwa.
Na Juliet Wekesa