Kufuatia uteuzi wa mawaziri na Rais William Ruto hapo jana, wananchi mbali mbali wameweza kutoa
hisia au maoni yao kuhusiana na uteuzi huo. Wengine wamefurahia sana kupewa nafasi mbalimbali
huku wengine wakilalamikia kutopewa nafasi. Kwa mfano, wakazi wa Nandi wamelalamika wakisema
kwamba Rais “amewafinya” na ni kinyume na matarajio yao.

Wakazi wa maeneo ya magharibi na hususan Bungoma kwa upande mwingine waliweza kufurahia sana
kwa kusema kwamba wamewakilishwa vyema, ikizingatiwa kwamba Musalia Mudavadi na Moses
Wetangula ni wa eneo hilo.

Wakazi wa Samburu pia walitoa hisia mseto wakisema kwamba walitarajia kupewa nafasi na Waziri wa
usalama angetoka eneo hilo. Wanaona ni kama wamesahaulika.

Wengine walisema kwamba vijana hawajawakilishwa kama vile Rais aliwaagiza huku wengine wakisema
kwamba wanawake wamewakilishwa vyema na hivyo kuna usawa wa kijinsia.

Kilichobaki sasa ni kusubiri mawaziri hao kupigwa msasa au kuhakikiwa ili waanze rasmi kutekeleza
majukumu yao.

By Calvin Angatia

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here