
Kampuni ya Sportpesa imezindua rasmi msaada wake kwa Gor Mahia mara tena baada ya muda wa miaka mitatu. Kampuni hiyo ilisitisha msaada wake kwa Kogalo Agosti 2019 kufuatia mzozo kati ya kampuni hiyo na serikali ya kitaifa. Wachezaji wa Gor Mahia sasa wanafuraha kubwa, ari na matumaini ya kurejea kileleni kwenye jedwali la soka nchini jinsi nahodha wa klabu hiyo anavyosimulia.
Mwaniaji wa kiti cha useneta katika kaunti ya Bungoma Lemdrix Waswa ameanza kuandaa mashindano ya soka kwenye kaunti huku akianzia nyumbani kwake katika eneo bunge la sirisia. Waswa ameapa kuendelea na msururu wa michezo kaunti nzima akiwa na lengo la kuwaleta vijana pamoja na hivyo kuepukana na vitendo hasi kama vile kujihusisha na mihadarati. Aidha ametoa wito kwa wakazi wa kaunti ya Bungoma kusimama naye wakati wa uchaguzi huku akikiri imani yake ya kuibuka wa kwanza katika uchaguzi huo.
Ughaibuni ni kuwa  Uingereza walitoka sare ya 3-3 dhidi ya Ujerumani katika mechi ya kusaka ubingwa wa ligi ya mataifa barani Ulaya.hii leo katika mida ya saa nne kasorobo, itakua kibarua kati ya Italia na Ureno.Â
Na Brian Simiyu