
Rais William Ruto ameongoza kikao cha kwanza cha baraza la mawaziri katika ikulu ya Narobi. Mawaziri wote wamehudhuria mkutano wa leo, wakiwemo wale waliojitokeza wazi wazi kupinga kuchaguliwa kwa Ruto kuwa rais.
Rais William Ruto aliongoza kikao chake cha kwanza cha baraza la mawaziri katika ikulu ya nairobi mkutano ulihudhuriwa na mawaziri wanaoondoka ambao walihudumu chini ya serikali ya rais mstaafu Uhuru Kenyatta.
waziri wa usalama Fred Matiang’i , waziri wa habari na mawasiliano joe mucheru na waziri wa mazingira Keriako Tobiko waliokuwa wapinzani wakuu wa Ruto wa uchaguzi pia walihudhuria mkutano huo
Aliyeonekana kutohudhuria kikao cha baraza la mawaziri ni waziri asiyekuwa na wizara maalum Raphael Tuju,
Kulingana na ilani ilitolewa na mkuu wa utumishi wa umma Joseph Kinyua mawaziri wote na makatibu wa kudumu waliohudumu katika serikali ya rais mustaafu Uhuru Kenyatta wataendelea kuwa afisini hadi wengine watakapoteuliwa.
Baraza hilo linakutana wakati taifa linakumbana na changamoto chungu nzima zikiwemo mfumko wa bei za bidhaa, baa la njaa na hali mbaya ya nchi kiuchumi.
Mkutano huo unatarajiwa kujadili masuala mbali mbali yakiwemo utovu wa usalama katika baadhi ya maeneo ya nchi na mbinu na mwafaka za kupunguzia wananchi mzigo wa gharama ya maisha.
Na Marion Wafula.