Wafanyi biashara wadogo  katika maeneo la Nyanza  katika ufuo wa ziwa la Victoria eneo la Sinyenye Port Victoria wanamomba Rais William Ruto  kutimiza ahadi aliyowapa  akina mama mboga na wanabodaboda.

Wachuuzi hao wanaitaka serikali kutimiza ahadi ilizotoa za kuinua maisha ya mahasla katika kipindi cha
kampeni. Kundi la wafanya biashara hao linasema jambo muhimu hivi sasa ni mikopo itakayo wawezesha
kuagiza malighafi za biashara zao kutoka taifa jirani la Uganda ilikujiendeleza kimaisha.

Naomi Barasa mmoja wa wafanyabiashara analalamikia hali ngumu za kibiashara na gharama za
maisha huku akidai bidhaa mbalimbali haswa nafaka ina bei ghali na kupatikana kwao si rahisi.

Kulingana na Miriam Ongoma, wafanya biashara wengi wa eneo hilo walimpigia kura rais William ruto
alipoahidi kuzingatia maswala yao na hivyo basi wanamrai kutimiza ahadi hizo. 

Na Emmaculate Wamalwa

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here