
Kizaazaa kimezuka ndani ya chama cha ODM hii ni baada ya vijana wa chama hicho kulalamikia
kutengwa na uongozi wa chama hicho haswa katika ugavi wa nyadhifa mbalimbali.
Umoja wa chama hicho cha ODM ambacho ni cha miaka kumi na saba kinatishiwa kufuati vita vinavyo
zuka dhidhi wa ugavi wa nyadhifa mbalimbali.haya yanajiri wiki moja baada ya kinara wa Azimio la
umoja Railla Odinga kumkabidhi mbunge wa Ugunja opiyo wandayi uongozi wa wengi wa Azimio katika
bunge la kitaifa jambo ambalo lilimfanya mwenyekiti wa ODM kuzua taharuki kuhusu uamuzi wa
kutomchagua licha ya hadhi wake kwenye chama hicho.
Baada ya hayo viongozi vijana katika ODM wakiongozwa na mbunge wa Embakasi mashariki Babu
Owino wameibua tetesi wakidai kinara wao Raila Odinga amewatenga. Kupitia kwa mtandao wa twitter
Babu Owino amehoji ni kwa nini chama hicho kimemkabidi John Mbadi uongozi wa kamati ya uhasibu
wa mali.
Seneta wa Narok Ledama Ole Kina amemuunga mkono babu owino huku akihoji ni kwa nini chama
hicho hakina ajenda ya kulea vijana ambao wamepigania chama hicho kwa muda mrefu.
Haya yakijiri,chama hicho kupitia kwenye mtandao kimepuzilia mbali tetesi za mgogoro.
Story by Emmaculate Wamalwa