
Kabla ya mkutano wa kilele wa hali ya hewa utakaofanyika mnamo November mwaka huu nchini Misri, wanahabari kutoka kote Afrika walijumuika jijini Kigali, Rwanda kujadiliana kuhusu mambo muhimu ambayo watahitaji yashughulikiwe katika mkutano huo wa Misri.
Mambo hayo yataweza kusaidia nchi mbalimbali za Afrika. Wanahabari kutoka kote Afrika waliitwa wakaitika. Walijumuika jijini Kigali, Rwanda na haja kubwa ya mkutano huu ilikuwa ni kujadiliana baadhi ya mambo ambayo watataka yajadiliwe kwa upana katika mkutano wa Novemba kule Misri (Halmaarufu COP 27).
Suala ambalo walitilia mkazo ni suala la hali ya anga ya Afrika. Mkurugenzi wa Power Shift Africa, Mohammed Adow alieleza kwamba waafrika wanahitaji kujipangia mikakati yao ya kushughulikia masuala yanayowahusu kwanza kabla ya kutafuta usaidizi kwa wazungu, hasa kuhusiana na hali ya anga.
Masuala mengine yalihusiana na mazingira kama vile ukataji miti ovyo Afrika, uchafuaji wa mazingira, ukosefu wa maji ya kutosha na ukame.
Kilichobakia sasa ni mkutano huo wa Cop 27 kujadili masuala hayo kwa kina na jinsi watakuwa wanashughulikia janga la hali ya anga linalokumba Afrika.
Na Calvin Angatia