
Wadau mbalimbali kutoka mashirika yaliyo ya kiserikali na yasiyo ya kiserikali walikusanyika kwa maadhinisho ya siku ya amani mjini Eldoret. Gavana wa kaunti ya uasin gishu, Jonathan Bii na kamshna wa NCIC Sam Kona waliongoza hafla hiyo.
Hapo awali wakazi wa uasin gishu walikuwa na hofu huenda kukazuka ghasia katika kaunti hiyo wakati wa uchaguzi ndiposa tume hiyo ya ncic ikaandaa sherehe hizi ili kuwashukuru wakaazi wa eneo hii na wakenya wote kwa jumla kwa kudumisha amani.
Washikadau waliozungumza kwenye hafla iliyopangwa na wanafunzi wa vyuo mbalimbali waliwashukuru hasa vijana kwa kutokubali kutumiwa vibaya na wanasiasa.
Viongozi hao pia walimtaka rais william ruto kuwajumuisha wale ambao hawakumpigia kura katika serkali yake
Na kwingineko, eneo la Mathare katika kaunti ya Nairobi, wanaharakati wa kutetea haki za kibinadamu walishiriki katika maandamano ya amani ili kuadhimisha siku hii waliongozwa na naibu kamshna wa eneo la Mathare Benson Mbivi.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni “komesha ubaguzi wa rangi, dumisha amani.”
By Marion Wafula