“SI MKAAJI WA HAPA” KIZAZAA CHAZUKA POKOT.

0
11

Kizaa kilizuka nje ya majengo ya bunge la kaunti ya West Pokot baada ya wakaazi wa eneo hilo kumzuia mwakilishi wadi aliyeteuliwa na chama cha UDA kuingia bungeni kula kiapo. Wakaazi hao waliojawa na gadhabu wanadai kuwa mwakilishi wadi huyo si mkaazi wa kaunti hiyo na uteuzi wake hauafa.

Mwakilishi wadi huyo alizuiliwa kula kiapo kizazaa hiki kilichangiwa na wakaazi ambao wanadai kuwa mmoja aliyeteuliwa na chama cha uda sio mkaazi wa Pokot Magharibi. Hivyo basi kuwanyima wanaostahili kuwa waakilishi wadi maalum.

Sio hao pekee waliokuwa na ghadhabu pia wanaoishi na ulemavu, wanadai kuwa hawakupewa nafasi katika bunge la kaunti ya Pokot Magharibi. Wanasema kuwa masuala yanao walenga yakakosa kufuatiliwa.

Baada ya tumbo joto kutulia waakilishi wadi na waliochaguliwa waliapishwa kuanza majukumu yao ya kuunda sheria na kujadili misuada muhimu. Japo mwakilishi wadi Ahmed Desi Issack, kuzuiliwa nje na wakaazi hao kutaka kubadilishwa kwa uteuzi wake. Ahmed alishikilia kuwa yeye ni mpiga kura na mkaazi wa kaunti ya Pokot Magharibi.

YouTube player
Na Faith Njerwe

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here