Mwanariadha mwenye kasi kubwa zaidi Afrika Ferdinand Omanyala hii leo ametuzwa kama mwanamichezo bora nchini mwezi Agosti. Hili linatikana na ushindi mkubwa alioutwaa kwa kushinda nishani ya dhahabu afrika na vilevile kuibuka wa kwanza kwenye mashindano ya madola kula Birmingham Uingereza.
Kwingineko mwenyekiti wa FKF Nick Mwendwa sasa yuko taabani. Siku moja tu baada ya kurejea ofisini. Hapo jana Nick Mwendwa alirejea kazini kinyume na matarijio ya wengi huku akisema ujio wake ni mwamko mpya wa uhuru wa soka nchini. Vile vile ombi la mwenyekiti huyo kwa mahakama kuu nchini kutuoilia mbalituhuma zinazommkumba zikiwemo za ufisadi limegonga mwamba.
Hatimaye Malkia Strikers wametua Uholanzi tayari kea mashindano ya kusaka ubingwa wa mchezo wa wavu duniani. Vipusa hao wamekua wakikita kambi nchini brazil kwa miezi mitatu wakifanya mazoezi kabla ya kuelekea Serbia na kucheza mechi kadhaa za kirafiki kisha kupaa angani kuelekea uholanzi ambapo michuano hiyo itaandaliwa. Kwa mujibu wa washikadau mbalimbali pamoja na wachezaji, maandalizi yaoyamekuwa ya kufana na hivyo wako tayari kusajili matokeo ya kuridhisha. Wanadada hao wamo katika kundi moja na wenyeji wao. .