KENYA YAWEKA MIKAKATI KUZUIA EBOLA KUTUA NCHINI.

0
6
Taifa la Uganda limeendelea kuimarisha hali yake ya kiafya baada ya virusi vya Ebola kuripotiwa. Maafisa wa Afya Duniani, wakishirikiana na wale wa taifa hilo kudhibiti maambukizi . Taifa hilo kwenye taarifa yake mapema wiki hii, ilisema kuwa, mwanaume mwenye miaka ishirini na mine, alifariki katika eneo la Mubende kutokana na virusi hivyo.

Na katika kuhakikisha virusi hivyo haviingii nchini, wizara ya afya imebuni mikakati haswa maeneo ya mipakani na kwa wahudumu wa afya. Kwenye taarifa yake waziri wa afya Mutahi Kagwe, aliagiza kuimarishwa kwa uchunguzi wa dalili za ugonjwa huo maeneo ya mpakani. Aidha serikali imeagiza kupima watu walio hatarini ya kuambukizwa ugonjwa, wakiwemo wasafiri, madereva wa treli, na wahudumu wa afya.

Wanaofanya kazi kwenye vituo vya afya pia wameagizwa kupewa mafunzo kuhusiana na virusi hivi. Na katika kuafikia maagizo haya, maafisa katika kaunti ya Busia wameanza kuweka mikakati ya  tahadhari.

Kaimu afisa wa afya kaunti ya Busia Melisa Lutomia, amesema wameanza kuwapima watu wanaongia mpakani. Aidha wakaazi wa eneo hilo wameingiwa na kiwewe kuhusu maambukizi. Daktari lutomia hata hivyo amesema wanashirikiana na idara nyingine za usalama  na uhamiaji kuhakikisha hali inaimaishwa zaidi.    

Na Joram Kitui

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here