
Wataalamu wa magojwa wa saratani kote nchini wamefanya kongamano la nane la kila mwaka la kisayansi katika hoteli ya Grand Royal swiss katika kaunti ya Kisumu kuzungumzia maswala ya ugonjwa wa saratani .
Tunapoelekea Mwezi wa oktoba ambao ni mwezi wa kuhamasisha wananchi kuhusu ugonjwa wa saratini, waatalamu hao wamehuduria kongamano hilo wakiongozwa na mwenyekiti Roselyn Okumu ili kujadili jinsi ya kuwashirikisha na kuwawezesha wauguzi kushiriki katika kudhibiti na kuzuia saratani.
Roselyn ameeleza kuwa kuna aina mbalimbali ya saratani ambayo imekuwa tatizo kubwa nchini
Kenya.
Kutibu ugonjwa wa saratani umekuwa bei ghali ambapo watu wengi wameshindwa kukimu, aidha kulingana na  mwenyekiti huyo, serikali imejisatiti kupambana na ugonjwa
huo.
Kwa mengi zaidi tazama video ifwatayo.
Na Emmaculate Wamalwa