UDM, HAKUNA KIZUIZI KUONDOKA AZIMIO.

0
6

Hali ya utata katika muungano wa Azimio la Umoja One Kenya inazidi kutokota huku baadhi ya vyama vilivyosaidia kuunda muungano huo vikisema kuwa vipo katika muungano wa kenya kwanza, chama cha UDM kinachoongozwa na seneta wa Mandera Ali Roba kinasema kuwa hakina hati zozote kutoka kwa muungano wa Azimio na hivyo basi hakuna kizuizi chochote cha kusalia kwenye, muungano huo.


UDM inasema kwamba ni sharti kuyaweka wazi yaliyomo ndani ya makubaliano ya muungano kwa wahusika wote, aidha roba anasema kuwa uamuzi wa chama hicho kujiondoa kutoka Azimio ulifanywa hata kabla ya uchaguzi mkuu.

Hali hii ni sawia katika chama cha pamoja African Alliance cha amason kingi ambacho kinasema kuwa kiko katika muungano wa kenya kwanza kisheria chama cha UDM kina wabunge saba huku cha paa kikiwa na wabunge watatu katika bunge la kitaifa idadi ambayo inaumuhimu mkubwa sana kwa nguvu za Kenya kwanza.

Miungano yote miwili Azimio la Umoja na Kenya Kwanza ikidai wingi katika bunge hilo,kwa mustakabali wake msajili wa vyama vya kisiasa Ann Nderitu anasema kuwa swala hilo liko mikononi mwa spika wa bunge la kitaifa ambaye anafaa  kufanya uamuzi huo  

Na Juliet Wekesa

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here