TAASISI YA UTAFITI WA BAHARINI NA UVUVI YAVUMBULIWA.

0
7

Taasisi ya utafiti wa baharini na uvuvi (KMFRI) imevumbuliwa huku ikipania kutumia nzi aina ya black soldier kwa uzalishaji wa chakula cha mifugo na samaki. Mabuu yanayoanguliwa na nzi hao hulishwa uchafu uliooza kutoka baharini na hata kwenye miji na kisha wadudu hao hutumiwa kutengeneza chakula cha mifugo pamoja na samaki.

Kulingana na James Njiru, mkurungenzi mkuu wa KMFRI,wadudu hao wana kiwango cha juu cha virutubishi kama protini na wanaweza kulishwa samaki na kuku wakiwa hai. NEMA vilevile wameahidi kushirikiana na serikali ili kuboresha usafi nchini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here