MLIPUKO WA EBOLA UGANDA.

0
4

Kisa cha ugonjwa wa Ebola unaoambukizwa kupitia virusi kimeripotiwa nchini Uganda na wizara ya afya. mlipuko huo ni wa aina ya ‘Sudan strain’ na mara ya mwisho kuripotiwa ilikuwa mwaka wa elfu mbili na kumi na mbili (2012).


Kisa kimoja cha ugonjwa hatari wa Ebola kimeripotiwa nchini Uganda. Mgonjwa huyo ni mwanaume wa miaka ishirini na minne na ilisemekana kuwa alionyesha dalili za ugonjwa huo na akapelekwa katika kituo cha afya ambapo alifanyiwa majaribio ya maabara na kisha kupatikana kuwa ni Ebola. Mwanaume huyo anatokea maeneo ya Mubende, inayopatikana kilomita mia moja hamsini magharibi mwa mji wa Kampala.

Kulingana na wizara ya afya ya Uganda, aina hiyo ya Ebola iliripotiwa mwisho mwaka wa elfu mbili na kumi na mbili. Inasemekana kuwa aina hii ni hatari sana na inaweza kuangamiza watu wengi sana kwa muda mchache sana.

Wizara ya afya ya Uganda ikiongozwa na Waziri Jane Ruth imewahakikishia wananchi kwa ujumla kwamba wawe watulivu na wizara iko tayari kushughulikia janga hilo kwa njia inayofaa ili kuhakikisha kwamba wananchi wako salama na hawataambukizwa.

Haya yakijiri, wakazi wa Busia katika mpaka wa Kenya na Uganda wametaka serikali ya kaunti pamoja na serikali kuu zichukue hatua ya haraka sana kuhusiana na mlipuko huo wa ebola.

Wakazi hao walijieleza kwamba wanahofia sana maisha yao kwa sababu wako katika mpaka na hivyo kuambukizwa itakuwa rahisi.

Wanataka serikali izindue chanjo ya ebola kama ile ya korona kama njia mojawapo ya kuzuia au kudhibiti ugonjwa huo na pia wanaoingia nchi hii kutoka Uganda waweze kupimwa kabla ya kuruhusiwa kuingia.

By Calvin Angatia

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here