KIANGAZI NCHINI.

0
13

Hali ya kiangazi imeendelea kuwatatiza wakenya wengi sana katika maeneo mbalimbali nchini, hasa maeneo ya kaskazini mashariki mwa Kenya. Hali hii imeleta njaa katika maeneo hayo na watu wengi wanaendelea kuaga dunia na hata pia mifugo. Maeneo hayo ni kama vile Kajiado na Marsabit.

Hali ya kiangazi imetatiza hata mifugo kwa kuwa hakuna nyasi na hata maji. Watu wengi katika maeneo hayo wanafuga mifugo kama vile ng’ombe na mbuzi na hivyo wanatafuta njia mbalimbali ya kulisha mifugo. Wengine wanaonelea kuuza ng’ombe ama mbuzi ili angalau wapate cha kutia mdomoni. Tatizo ni kwamba hata bei ya mifugo imeshuka chini san ana haiwezi kidhi mahitaji yao.

Ukosefu wa chakula huleta ugonjwa au hali ya utapiamlo. Ni wazi kwamba wengi wao wameambukizwa ugonjwa huu na hivyo basi mashirika mbalimbali kama vile Msalaba Mwekundu yanafaa yaingilie kati ili kuwanusuru walioathirika. Serikali pia inafaa ishughulikie suala hili haraka iwezekanavyo. Kulingana na Shirika la Afya Duniani, utapiamlo ni mojawapo ya sababu kuu zinazosababisha vifo vya watoto ulimwenguni kwa asilimia hamsini na tatu. Hii ni kumaanisha kwamba ni hatari sana na hivyo basi serikali ikishirikiana na wizara ya afya itafute njia mbadala za kudhibiti hali hiyo.

By Calvin Angatia

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here