WALEMAVU WATISHIA KUZUA MAANDAMANO.

0
6

Hii ni mara ya tatu ya kundi la watu wanaoishi na ulemavu kutishia kuenda mahakamani au kufanya maandamano baada ya kutengwa katika orodha ya uteuzi katika bunge la taifa na seneti.

Kundi la watu hawa katika kaunti ya Bungoma walikuwa w kwanza kulilia haki zao na kusema kuwa wametengwa na kusahaulika na viongozi wao wakidai kuwa wanataka maslahi yao yashughulikiwe na serikali itoe msaada kwao.

Baadaye kundi la kaunti ya Transnzoia lilitishia kufanya maandamano. Wakiwa na kikao na wanahabari walisema kuwa hatua ya vyama hivi kuwatenga katika orodha zao ni kinyume na sheria na haki ya kikatiba inasema kuwa wawasilishwe katika bunge.

Hali sawia ambapo kundi la watu hawa wanalalamika katika kaunti ya Uasin Gishu. Kundi hili lilimwomba rais wa kenya kushughulikia hali yao kwa sababu rais William Ruto ni mkaazi wa kaunti hiyo na ana roho ya utu. Walitishia kufanya maandamano na kuenda bungeni kupiga kambi huko iwapo hawatasikilizwa.

Kabla ya uchaguzi, naibu wa mwenye kiti wa IEBC Juliana Cherera alisema kuwa mikakati yakuongeza kundi la watu wanaoishi na ulemavu umeshughulikiwa na kuongezwa katika uchaguzi lakini ahadi hiyo hijatimizwa hadi sasa.

Lililobakia sasa ni kujua kama maslahi ya makundi haya yatashughulikiwa na masuala haya kutatuliwa.

By Marion Wafula

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here