
Wakati wa kampeni rais wa sasa William Ruto, alionekana kumsuta rais mstaafu Uhuru Kenyatta na kiongozi wa upinzani Raila Odinga kwa kile alikitaja kuwa muungano wao almaarufu handshake ndicho chanzo kikuu katika kupanda kwa gharama ya maisha nchini, aidha aliwarai wakenya kumpigia kura kwani yeye tu ndiye angekuwa mkombokozi wa watu wa tabaka la chini almaarufu hustlers.
Ila siku chache baada ya kuapishwa kwake gharama ya umeme na mafuta imeongezeka.
Ongezeko la bei ya umeme, lililochapishwa mwezi jana, bila kutangazwa, limeanza kutekelezwa wiki hii. Mamlaka ya kudhibiti kawi na petroli epra, ilichapisha ongezeko la bei ya umeme kwa asilimia 21, ikiongeza gharama ya kilowati moja, kutoka shilingi 21, hadi shilingi 25.3, gharama ya mafuta ya kuzalisha umeme, nayo ikiongezeka kutoka shilimgi 4.63 hadi 6.8.
Ni mabadiliko yanayojiri, miezi tisa, baada ya rais msataafu kuagiza kupunguzwa kwa bei ya umeme, kwa asilimia 15. Aidha hakuna sababu imetolewa ,kwa ongezeko hilo.
Wakati huo huo, bei ya mafuta imeongezeka, tangazo hilo linafwatia baada ya rais william ruto, kuondoa ruzuku ya petroli, iliyokuwa ikimsitiri mwananchi, huku ruzuku ya mafuta taa na dizeli ikipunguzwa.

Petrol sasa imeongezewa bei kwa shilingi ishirini, ikitarajiwa kuuzwa kwa shilingi 179.3, kutoka kwa shilingi mia moja 159.12. Dizeli sasa itauzwa kwa shilingi 165, kutoka kwa shilingi 140. Nayo mafuta, ya taa kuuzwa kwa shilingi 147.24, kutoka kwa shilingi 127.24.
Tayari hazina ya kifedha ya kimataifa IMF, ilikuwa imedokeza kuondolewa kwa ruzuku hiyo, kufikia mwezi oktoba, na kwa hivyo wakenya kulazimika kulipa gharama yote.
Swali ni je, rais William Ruto ana mpango upi katika sekta hiyo?
Na Joram Kitui