Huku ulimwengu ukiadhimisha siku ya masomo ya uzeeni duniani, wananchi wameshauriwa kutilia maanani elimu kwa watu wazima huku serikali ikitakiwa kufadhili masomo haya kikamilifu. Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Siku hii ya kusherehekea kuadhimisha kisomo nchini iliongozwa na naibu kamishna wa Webuye Magharibi Ediang’ Nanok huku akisema kuwa malengo ni kuhamasisha jamii kuendeleza kisomo. Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â Â
Chifu wa Miendo Carol Lwiki akielezea mfano wa yeye kurudi shuleni kidato cha pili akiwa na miaka thelathini na baadaye kufuzu huku akiwapa motisha wananchi wengine. Mwalimu anayesiamamia masomo ya utu uzima bwana Oscar Tinde akisema kuwa aina ya masomo yanayotolewa ni masomo ya kawaida na masomo ya kujiendeleza. Changamoto kuu ikiwa waalimu wachache wa kuendeleza kisomo hicho. Â