
Kabla wakenya kushiriki katika uchaguzi mkuu wa agosti tisa, viongozi waliokuwa wakiwania viti mbalimbali walikuwa wakifanya kampeni zao katika maeneo mbalimbali nchini. Kwenye kipindi hiki cha kampeni, misimu mbalimbali ilizuka, wangine wakiikubali baadhi ya misimu hiyo, na wengine kuipinga. Mfano ya misimu hii ni kama vile neno ‘sipangwingwi’ neno ambalo lilikuwa likitumika na rais mteule kipindi hicho akiwa bado ni naibu wa Rais William Ruto na mrengo wake wa kenya kwanza kwa jumla kwenye kampeni zao, lakini kisha baadaye ukaonekana kupingwa na baadhi ya viongozi, kwa kile walichodai kuwa ni neno la chuki
Baadhi ya maneno tatanishi kwenye msimu huo wa kampeni, ni maneno ya ‘deepstate’ na ‘system’ ambayo yalikuwa yakitumiwa kumaanisha watu wenye nguvu au mamlaka makubwa serikalini. Maana halisi ya neno ‘deep state’, ni kikundi cha watu au wanajeshi, ambao ni wanachama wa mashirika ya serikali, wanaoaminika kuhusika katika upotoshaji au udhibiti wa sera za serikali. ‘system’ nayo vilevile, ikionekana kuwa kikundi cha watu flani mashuhuri, ambao wanafanya kazi pamoja ili kuona kwamba wanafanikisha lengo au nia yao serikalini. Sasa swali wanalojiuliza wananchi wa kenya ni je, ‘deep state’ na ‘system’, ni akina nani hapa nchini?
Wakati maneno hayo mawili yalipokuwa yamepamba moto kwenye kipindi hicho cha kampeni, rais mteule William Ruto alijitokeza na kupinga kasumba hiyo ya ‘deep state’ na ‘system’, akisema kuwa hakuna watu kama hao nchini, na hawawezi kuwepo wakati yeye kama naibu wa rais wa kipindi hicho akose kuwatambua.

Tukiangalia tu kwa mbali, ‘deep state’ na ‘system’ hapa nchini kama iko, inafaa kuhusisha viongozi wote wawili wakuu, ambao ni rais uhuru kenyatta na naibu wake william ruto, kwani hao ndio wanaojua mambo mengi yanavyoenda hapa nchini. Kitendo cha Dkt William Ruto kupinga uwepo wa asasi hizo mbili, ni kumaanisha kuwa kuna uwezekano mkubwa kuwa asasi hizo hazipo hapa nchini, ama zipo lakini yeye hajihusishi nazo.
Rais Uhuru Kenyatta, ambaye alikuwa anaegemea mrengo wa azimio kwenye uchaguzi mkuu uliopita pamoja na kinara wa mrengo huo Raila Odinga, walikuwa wakichukuliwa kama wanachama wa asasi hizo, kwa kile kilichoonekana wakati wa kampeni zao, na ukaribu wao pia.
Kwenye chaguzi mbalimbali ambazo viongozi hao wawili walikuwa wakipingana na dkt william ruto, ikiwemo ile ya BBI, Ruto alionekana kushinda chaguzi hizo, na kuacha maswali mengi kwenye vichwa vya wakenya, kama ‘deep state’ na ‘system’ zinaushawishi wa kiwango gani kwa wananchi, kwani hata kwenye uchaguzi mkuu wa agosti tisa, Ruto bado alishinda na kuicha kasumba hiyo ya ‘deep state’ na ‘system’ ikikosa nguvu.

Baada ya mrengo wa Azimio ambao ulikuwa unahusishwa na asasi hizo za ‘deep state’ na ‘system’ kubwabwa na mrengo wa kenya kwanza ambao ulikuwa unajitenga na asasi hizo, swali ni je? ‘deep state’ na ‘system’ ziko hapa nchini na zinaushawishi kwa wakenya, au ni kasumba tu ambazo wakenya wamezieka kwa akili zao? Unaweza kutupa maoni yako kupitia youtube channel ya runinga ya tandao ambayo ni, Tandao Tv Kenya ama kwa ukurasa wa facebook Tandao Tv Kenya.
Na David Amani