Mwaka wa elfu mbili kumi na saba, mahakama ya upeo nchini kenya,
iliandikisha nchi hii katika historia ya kuwa taifa la kwanza barani afrika,
kwa upinzani kushinda katika kesi ya kupinga uchaguzi wa rais, taifa
likiagizwa kufanya uchaguzi mpya baada ya Raila Odinga kupinga ushindi wa
rais Uhuru Kenyatta. Katika kesi hiyo, david kenani Maraga, alitangaza kuwa,
uchaguzi wa Kenyatta ulikuwa kinyume cha sheria, majaji wanne wakiunga
mkono uamuzi huo dhidi ya wawili wa mahakama ya upeo.
Idara ya mahakama ilimiminiwa sifa kutokana na hatua hiyo, wakenya
wakihisi mwamko mpya katika uhuru wa mahakama. Rais Kenyatta
alitangaza kuheshimu tangazo la hilo japo akakiri kutokubaliana na uamuzi
huo.
Miaka minne baadaye, Rais Kenyatta akiwa na Raila Odinga, Kalonzo
Musyoka, Gideon Moi na wengine, alikumbana na pigo jingine baada ya
mchakato wao wa kubadili katiba kupitia BBI, kugonga mwamba, mahakama
ya upeo ikidumisha uamuzi wa Mahakama za Juu na Rufaa.
Mahakama mara si moja imeamrisha serikali kumruhusu na kumwezesha
mwanasheria miguna miguna kurejeshwa nchini, baada ya kufurushwa
kwake nchini mwaka elfu mbili kumi na nane, kutokana na kuhusika kwake
katika kiapo cha Raila Odinga, baada ya uchaguzi mkuu.
Oktoba mwaka jana mahakama vilevile, ilitangaza mpango wa kisasa wa
usajili wa wakenya (Huduma namba) kuwa haramu na kuongeza kuwa
mpango huo, ulikiuka sheria inayohusiana na usiri wa Wakenya.
Mei mwaka jana mahakama ya juu ilitangaza kuwa, wakuu mia moja ishirini
na tisa wa mashirika ya kiserikali, (Parastatal bosses) waliochaguliwa na
Rais Kenyatta ni kinyume cha sheria.
Mahakama ya juu vilevile Februari mwaka elfu mbili kumi na saba, ilitupilia
mbali mpango ya serikali kufunga kituo cha wakimbizi cha Dadaab. Maamuzi
ya idara ya mahakama kukinzana na matakwa ya serikali hayajazaliwa enzi
za Maraga wala Martha Koome kwani mwaka elfu mbili kumi na moja,
mahakama ilifutilia mbali hatua ya aliyekuwa rais Mwai Kibaki kuwateua
maafisa wa mahakama ikisema alikiuka katiba. Rais Uhuru oktoba mwaka
jana alidinda kuwateua majaji sita wa mahakama akiwemo George Odunga
licha ya kupewa makataa ya siku kumi na nne na mahakama ya juu, kufanya
hivyo.
Siku chache zilizopita, mahakama ya upeo imedumisha uchaguzi wa William
Ruto kuwa raius wa Kenya, licha ya juhudi za Kenyatta kumpigia debe
Odinga. Katiba ya Kenya inahitaji idara ya mahakama kufanya kazi yake bila
mwingilio wa vitengo vingine vya serikali, watu wote wakitakiwa kuiheshimu
sheria.


Na JACOB MACHESO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here