Katika malalamishi ya kwanza ambayo walalamishi walidai ya kwamba mshindi hakufikisha asilimia hamsini na moja, Korti iliwajibu kwa kusema kuwa tume ya IEBC ilitumia mbinu zingine kumtambua mshindi. Katika lalamishi lingine ambapo walidai kuwepo na utofauti katika fomu thelathini na nne zilizopigwa picha na zile zilizochapishwa, korti ilisema kuwa madai hayo hayakuwa ya kweli.Katika lalamishi lingine ambapo walalamishi walidai kuwepo kwa udukuzi wa mitambo ya IEBC korti ilisema kuwa madai hayo hayakuwa ya kweli wowote. Katika uamuzi wa mwisho wa korti,mahakama ilishikilia ushindi wa Rais mteule William Ruto.Baada ya kutangazwa na mahakama kuwa mshindi katika kesi hiyo Rais mteule William Ruto aliwahutubia wakenya Na kuahidi kuwatumikia kwa usawa.


Na Diana Eboso

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here