
Shirikisho la soka nchini FKF limeahirisha kuanza kwa ligi hiyo, kwa minajili ya kuapisha serikali mpya kushika usukani. Awali ligi kuu ya soka nchini ilikuwa imeratibiwa kuanza jumamosi wiki hii na kisha kuahirishwa kwa majuma mawili yajayo. Kocha mkuu wa klabu ya AFC Leopards almaarufu Ingwe amekashifu uamuzi huo na kudai kuwa umemharibia ratiba na mipango yake kwenye klabu hiyo.

Na Brian Simiyu