Asilimia kubwa ya wakenya wamekuwa wakielekeza macho yao  kwenye kwenye uamuzi wa mahakama  ya upeo, kuhusiana na matokeo ya kesi ya urais uliopita. Baada ya Jaji Mkuu Martha Koome kutoa uamuzi wa mahakama ambao umeidhinisha ushindi wa rais mteule William Ruto, waakazi mbalimbali wa kaunti ya Bungoma wamejitokeza na kutoa  maoni yao.

Baadhi ya wakaazi hao wamempongeza rais mteule William Ruto na pia kumrai kushughulikia swala la uchumi, wakisema kwamba watu  wa Bungoma walimpigia kura wingi.

Aliyekuwa naibu spika wa bunge la kaunti ya Bungoma ambaye ni mwakilishi wadi ya Siboti Wamusai Simiyu , pia amejitokeza na kumpongeza Ruto, huku akisema kwamba licha ya kuwa alikuwa wa mrengo wa Azimio, amekubali maamuzi ya mahakama.

Simiyu amemtakia kheri seneta wa Kaunti hiyo Moses Wetangula kwenye kinyang’anyiro cha uspika wa Bunge la Kitaifa, akisema kwamba baadhi ya viwanda vilivyofifia kikiwemo kile cha Nzoia, na pia kupunguza bei ya mbolea.pia itawafanya waakazi wa Bungoma kutambulika.

Aidha waakazi hao wamemtaka rais mteule kufufua baadhi ya viwanda vilivyofifia kikiwemo kile cha Nzoia, na pia kupunguza bei ya mbolea.

YouTube player

Na David Amani

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here