“Siku zote msimamo wetu umekuwa wa utawala wa kufwata sheria na katiba. Kuhusiana na hili, tunaheshimu maoni ya mahakama, ingawa hatukubaliani kamwe, na uamuzi wake.” Ndiyo maneno aliyosema Raila Odinga, saa chache tu baada ya mahakama ya upeo kushikilia matokeo ya tume huru ya uchaguzi na mipaka, IEBC kuwa, kuwa mpinzani wake, William Ruto alichaguliwa kihalali tarehe tisa Agosti.

Katika taarifa kwa vyombo iliyotiwa sahihi na Raila Odinga, mrengo wa Azimio la umoja umekiri kuheshimu maamuzi ya mahakama, licha ya kutokubaliana na maamuzi yaliyotolewa kuhusu hatma ya Odinga debeni.

Tangazo hilo limeoana na mtazamo wa mawakili waliomwakilisha Odinga na Karua kortini, James Orengo na Phillip Murgor wakisema ushahidi wao ulikuwa wa kutosha kubatilisha uchaguzi wa Ruto, kinyume na uamuzi wa majaji saba wa mahakama ya upeo kuwa, ushahidi uliotolewa katika maswala kadhaa kotini hukutosha kubatilisha ushindi wa Ruto.

Majaji wa kesi ya uchaguzi

Rais wa mahakama ya upeo, Martha Koome vilevile ametangaza kuwa ushahidi uliotolewa na baadhi ya waliopinga uchaguzi wa Ruto, wakiongozwa na  Celestine Opiyo na Arnold Oginga chini ya uwakili wa Julie Soweto na wengineo, ulikuwa wa uongo, akiongeza kuwa ni kinyume na sharia na ni hatia inayoweza kuvutia adhabu ya kikatiba.

James Orengo, anayehudumu kama gavana wa siaya hata hivyo anaonekana kutokata tamaa, akionyesha matumaini kuwa ipo siku mtazamo wa Azimio mahakamani utakumbatiwa na maswala yaliyoibuliwa na Odinga yatatiliwa maanani.

YouTube player

Na Jacob Macheso

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here