MAWAKILI HAWA NI KINA NANI?

0
24

Baadhi ya mawakili waliosimamia kesi ya uchaguzi wa rais ni Fred Ngatia akisimamia rais mteule William Ruto, James Orengo akiwasilisha kinara wa Azimio la umoja Raila Odinga na Githu Mwigai akiwakilisha kiongozi wa IEBS, wafula chebukati watoa mawasilisho yao ya mwisho kabla wa uamuzi ya majaji wakuu

Siku tatu baada ya uchaguzi wa urais, kinara wa azimio la umoja Raila Odinga aliwasilisha malamishi yake katika mahakama kuu akidai kuwa kura za urais hazikuhesabiwa kwa haki. Alishataki mpizani wake ambaye ni rais mteule William Ruto na kiongozi wa IEBC Wafula Chebukati kwa wizi wa kura.

Baadhi ya mawakili waliowasilisha Bwana Raila Odinga ni, James Orengo.

James Orengo ni mmoja kati ya mawakili nchini kenya waliohitimu cheo cha washauri wakuu.alisoma katika chuo kikuu cha Nairobi na kuhitimu shahada katika sheria. Alijiunga na shule ya sheria na baadaye kukubaliwa kati baraza la sheria la kenya. Orengo alikuwa mbunge wa Ugenya kutoka mwaka wa 1992 hadi 1997, aliwania kiti cha urais mwaka 2002 na kupoteza kiti hicho kwa Marehemu rais wa zamani Mwai Kibaki, alikuwa katibu wa baraza la waziri wa ardhi kutoka mwaka 2008 mpaka 2013. Katika mwaka wa 2o13 alikuwa seneta wa kaunti ya Siaya. Alishinda kiti cha ugavana katika uchaguzi wa tarehe 9 agosti.

Katika uwasilishaji wa mwishi Orengo alisihi mahakama iadhibu IEBC kwa kutojali.

Mmoja kati ya mawakli aliyewasilisha rais mteule William Ruto katika mahakama makuu ni Fred Ngatia, Ngatia ni mojawapo wa washauri wakuu nchini kenya, alizaliwa mwaka wa 1956 kaunti ya baringo, ana miaka 41 ya uzoefu kama mtetezi.

Amehitimu shahada ya juu katika falsfa, shahada ya juu katika sheria, uzamili katika sheria na shahada katika sheria.Ngatia awakilisha rais Uhuru Kenyatta katika mahakama mara mbili.Ngatia ni mwanabiashara ambaye alikuwa anamiliki biashara zake .Ngati alikuwa kwenya mahojiano ya utafiti wa jaji mkuu nchini kenya

Katika uwasilishaji wake wa mwisho katika mahakama, Ngatia alisihi jaji mkuu kuzingatia yaliyotokea mwaka wa 2017 baada ya kurudia kupiga kura.

Na Marion Wafula

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here