Je, unamfahamu kwa utendeti jaji mkuu wa Kenya na naibu wake? Hapa nimekuandalia Makala kuhusiana na maisha ya wawili hawa wakiwa ni baadhi ya majaji wanaoisikiza kesi ya uchaguzi ya urais katika mahakama kuu ya Kenya.

Jaji juu Martha Karambu Koome alizaliwa mwaka wa Elfu moja mia tisa sitini  katika kijiji cha kithui kaunti ya Meru.

Koome alisomea shule ya msingi ya Mwiteria Meru kisha akajiunga na shule ya Chuka commercial baadaye akajiunga nashule ya wasichana ya Mugoiri Muranga alikosemea ‘A level’ yake kisha akajiunga na chuo kikuu cha Nairobi alikosemea shahada yake ya uwanasheria na kuhitimu mwaka wa elfu moja mia tisa themanini na saba.

Alihitimu na shahada ya uzamili ya sharia katika shule ya sharia ya Kenya baadaye alienda katika chuo kikuu cha London ambapo alisomea shahada ya uzamili ya sharia katika sharia ya kimataifa za umma na kuhitimu mwaka wa elfu mbili na kumi.

Alikua mshirika wa kisheria katika Mathege na mawakili wa Muchemi kuanzia mwaka wa elfu moja mia tisa themanini na nane hadi mwakaa wa elfu moja mia tisa tisini na mbili baadaye alianzisha kampuni yake ya mawakili kwa Jina Martha Koome and advocates,amehudumu kama mjumbe wa baraza kati chama cha sharia cha Kenya,pia kama Kamishna wa umoja wa Affrica,pia anahusishwa na katiba yam waka wa elfu mbili na kumi.

Alijiunga na mahakama mwaka wa elfu mbili na tatu ambapo alichaguliwa kama jaji wa mahakama kuu kisha akachukua nafasi ya jaji wa mahakama ya Rufaa kwanzua mwaka wa elfu mbili ishirini na moja .Alichaguliwa kuwa jaji mkuu na Rais Uhuru Kenyatta mwaka wa elfu mbili ishirini na mojatarahe kumi na tisa mei.

Philomena Mbete Mwilu alizaliwa mwaka wa Elfu moja mia tisa hamsini na  saba katika kaunti ya Makueni kiji cha Kilala . Alifuzu katika chuo kikuu cha Nairobi na kuchukuliwa kama wakili katika mahakama kuu ya Kenya katika mwaka wa elfu moja mia tisa themanini na nane

 Alihudumu kama mwanasheria katika  Muthoga Gaturu and company na baadaye kujiunga na Mutuunga advocates kisha kuhudumu katika kampuni ya bimya ya Jubilee akwa manaja kisheria  karani wa bodi ya kudhibiti umeme. Amehudumu kama naibu aajaji mkuu kutokea mwaka wa elfu mbili kumi na tisa mpaka sasa.

Na Diana Eboso

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here