Magavana wapya walioteuliwa kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti tisa na kulishwa viapo, wameianza kazi yao huku wengi wakionekana kufanyia marekebisho wizara mbalimbali, ili kuimarisha hali ya kaunti hizo.

Gavana wa Bungoma Keneth Lusaka, hii leo amekuwa akizuru hospitali tofauti tofauti za kaunti hiyo, kuangalia utendakazi wake na hali ya hospitali hizo. Gavana huyo ameahidi kuimarisha sekta hiyo ya afya, akisema kuwa jambo la kwanza kulifanyia kazi ni kuandika kazi madaktari zaidi

Lusaka pia amewahimiza wakaazi hao wa bungoma kuchukua bima ya afya, ambayo itawasaidia kupata matibabu kwa urahisi na bei nafuu

Akiongelea swala la mashine ya kukagua viungo vya mwili ya x-ray, Lusaka amesema kuwa atalifanyia kazi na kuhakikisha kuwa wananunua, kwani kaunti hiyo haina mashine hiyo muhimu

Gavana huyo pia ameongelea swala la ushirikiano na mashirika ya kigeni, na kusema kuwa watakuwa wanafanya kazi na shirika kama vile USSAID, na mengine ya Korea, ili kuimarisha sekta hiyo ya afya.

Na David Amani

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here