Mheshimiwa Susan Kihika ataihudumia kaunti ya Nakuru kama gavana wa tatu na wakaazi wa Naivasha wanagoja kuona jinsi atakavyoikabili baadhi ya miradi iliyoanzishwa na gavana aliyekuwepo. Miradi hiyo ni  pamoja na mrengo wa wagonjwa wa nje katika hospitali ya eneobunge la Naivasha ambayo itagharamu takriban shilingi milioni mia tatu thelathini na moja, mrengo wa wagonjwa wa nje katika hospitali ya mai mahiu ambayo itagharimu takriban shilingi milioni mia moja na kumi na bandari kavu ambayo rais mteulewilliam ruto aliahidi kuirudisha mombasa

Na katika kaunti ya Kilifi, gavana Gedion Mung’aro ameanza kazi yake kwa kuwafuta kazi maafisa wakuu waliomfanyia kazi mtangulizi wake Amason Kingi. Gavana Mung’aro amesema kuwa hatua hiyo inalenga kupanga upya utawala wake kwa utoaji huduma bora

Katika kaunti ya Machakos, gavana Wavinya Ndeti amewaomba wale ambao hawajachukua bima ya kitaifa ya afya(NHIF) kufanya hivyo ili wafurahie matibabu kwa bei nafuu

Katika kaunti ya embu, gavana Cecil Mbarire ameunda kikosi cha kazi cha kufufua sekta ya afya iliyofifia.

Gavana Susan Kihika

Kikosi kazi hicho ambacho kina watu sita kikiongozwa na mwenyekiti wa huduma za matibabu daktari Francis Kimani, kinapaswa kuja na mapendekezo na uvumbuzi unaolenga kurekebisha sekta ya afya iliyofifia katika muda wa mwezi mmoja. Wakati huohuo, gavana Mbarire anasema kuwa utawala wake ulikwa umejitolea kwa mamlaka ya usambazaji wa vifaa vya matibabu ya kenya (KEMSA) kulipa sehemu ya bili inayosubiriwa ya shilingi milioni arubaini na saba iliyoacha na utawala uliokuwepo

Na katika kaunti ya Migori, katibu wa kaunti hiyo Christopher Rusanus, amesema kuwa manifesto ya gavana mpya itaunganishwa na bajeti ya ziada ili kufanikishautoaji huduma chini ya utawala mpya

Na Diana Eboso

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here