Shinikizo limetolewa kutoka kwa mbunge mteule wa webuye mashariki Martin Pepela akiwarai wabunge wenza kutoka mkoa pana wa magharibi kuunga mkono azma ya seneta wa Bungoma Moses Wetangula kuwa spika wa bunge la kitaifa .Pepela sasa akitaka wabunge hao kuweka kando tofauti zao za kisiasa na kumuunga wetangula kulingana na mkataba wa serikali ya kenya kwanza.

Kwenye kikao na waandishi wa habari mjini Webuye Pepela amewataka wabunge hao kutoa mkoa wa magharibi kujukumika na kumteua seneta Wetangula kama spika wa bunge la kitaifa.

Pepela akisisitiza kuwa uteuzi wa Wetangula chini ya muungano wa Kenya kwanza una manufaa kwa jamii ya Luhya kwani seneta Wetangula atakua na mamlaka nchini Kenya na kuleta maendeleo eneo hili.

Kwa wakaazi wa Webuye mashariki,mbunge Martin pepela aliwahakikishia kuwa atahakikisha wakaazi wa eneo hilo wanapata manufaa kwenye serikali ya kitaifa na serikali ya kigatuzi mtawalia.

Na Aris Wanyonyi

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here